Gomes achekelea sare Sudan

SUDAN. KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema aliandaa kikosi chake vizuri kwa ajili ya kujaribu kupata ushindi katika mechi ya leo lakini imeshindikana.

Gomes alisema walifanya maandalizi ya kutosha bila ya kuwazara Al Merrikh kwa kuwa wamepoteza mechi mbili za awali.

"Hatukufanikiwa kupata pointi tatu ila tumepata moja ambayo imetufanya kufikisha pointi saba katika kundi si jambo baya," alisema.

"Tutajiandaa zaidi tena kwa umakini mkubwa katika mechi ya marudiano ambayo tutacheza siku chache zihazo nyumbani kwetu ili kupata ushindi na kufikisha pointi kumi," alisema.

"Tulishindwa kufunga bao katika mechi ya leo ingawa tulitengeneza nafasi za kufanya hivyo.

" Tuliingia na plani ya kucheza kwa kujilinda muda mwingi na kufanya nashambulizi ya kushtukiza ili kufunga bao la namna hiyo kutokana tupo ugenini.

"Katika kuzuia tulifanya vizuri ila kwenye kushambulia tulifanya vibaya kwa kukosa nguvu wachezaji wangu na kupoteza nafasi hizo," alisema Gomes.

"Nitakaa na wachezaji wangu kama familia ili kugundua tulishindwa wapi kufunga bao na katika mechi ya nyumbani tuweze kufanya hivyo na hilo linawezekana," aliongezea Gomes.