Hii hapa CV ya kocha Hitimana wa Simba

Saturday September 11 2021
cv hanspic

Kocha Hitimana Thiery

By Saddam Sadick

Dar es Salaam. Pamoja na ukimya wake Kocha Hitimana Thiery ambaye ambaye ametangazwa kuwa kocha msadizi wa Simba, kumbe anayo elimu ya kutosha kwenye soka na hata nje ya mpira kwani ana Leseni A ya Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) .

Pia Kocha huyo raia wa Rwanda na ni Mkufunzi wa Makocha anayetambuliwa na Caf, na nje ya Soka ana Shahada ya Biashara na Shahada ya Uzamili (Masters) kwenye Utawala.

Katika uzoefu wake amefundisha timu mbali mbali na kuwatoa wachezaji wengi wanaotamba kwenye soka la ushindani akiwamo Haruna Niyonzima (Yanga) na Meddie Kagere wa Simba.

Soma zaidi:Hitimana kuchukua mikoba ya Gomes

Timu alizowahi kufundisha ni Rayon Sports mwaka msimu wa 2003/4 na kipindi hicho, alikuwa akiwanoa wachezaji wengi akiwamo aliyewahi kuw Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma.

Pia msimu wa 2004/6, aliifundisha Light Stars Seychelle, ambapo katika kikosi chake walikuwamo, Bakari Malima, Peter Manyika na Djuma kabla ya kurudi Rayon msimu wa 2006/9 akiwano tena Djuma na Haruna Niyonzima, ambapo alikuwa akimsaidia Luc Eymael wa Yanga kwa sasa.

Advertisement

Timu nyingine ni Musanze FC (2009/10), AS Kigali (2010/12).

Kwa Tanzania amezinoa Namungo, Mtibwa na Biashara United.

Advertisement