Kadi ya Bluu kwenye soka inatumika hivi
Muktasari:
- Imebainishwa kuwa chombo cha kutunga sheria za soka International Football Association Board (Ifab), kimeidhinisha kuanza kutumika kwa kadi mpya katika mchezo wa soka ikizifuatia kadi za njano na nyekundu zilizoanza kutumika katika Kombe la Dunia la 1970.
Kadi ya bluu itatambulishwa leo kuanza kutumika kama sehemu ya majaribio ya ‘kapu la watenda madhambi’ kwenye mchezo wa soka.
Imebainishwa kuwa chombo cha kutunga sheria za soka International Football Association Board (Ifab), kimeidhinisha kuanza kutumika kwa kadi mpya katika mchezo wa soka ikizifuatia kadi za njano na nyekundu zilizoanza kutumika katika Kombe la Dunia la 1970.
Hatua hiyo ya mabadiliko itatangazwa na Ifab kama sehemu ya utaratibu mpya wa adhabu wa “kapu la watenda madhambi” ambalo litashuhudiwa wachezaji wakitolewa uwanjani kwa dakika 10 kama watafanya madhambi makubwa au kupinga uamuzi wa waamuzi. Yaani ukionyeshwa kadi ya bluu, hutolewi moja kwa moja, unakuwa umewekwa kwenye “kapu la watenda madhambi” nje ya uwanja kwa dakika 10, kisha unarudishwa mchezoni.
Chama cha Soka cha Wales kimepanga kuanza kuitumia kadi ya bluu kama majaribio ya protokali mpya ya “kapu la watenda madhambi” kwenye mechi za michuano ya vijana wadogo msimu huu, huku rangi ya bluu ikichaguliwa badala ya rangi kama ya machungwa ili kuitofautisha kabisa kadi zile zilizozoeleka za njano na nyekundu.
BLUU MBILI SAWA NA NYEKUNDU
Utaratibu huo mpya unaotangazwa leo utatumikia tu kuwaadhibu wachezaji wanaofanya madhambi ya kuzima shambulizi pamoja na kupinga uamuzi wa waamuzi, pamoja na kuthibitisha kwamba mchezaji ataonyeshwa kadi nyekundu kama ataonyeshwa kadi za bluu mbili wakati wa mechi au endapo atapata kadi moja ya njano na nyingine ya bluu.
Ligi za kulipwa za madaraja ya juu zitaepushiwa majaribio ya kadi hizo za bluu, lakini majaribio yanapaswa kuanza haraka iwezekanavyo Juni mwaka huu.
Majaribio yanaweza kujumuisha michuano kama Kombe la FA na Kombe la FA la wanawake na kadhalika, huku chama cha soka cha England kikijitolea kuanza kuijaribu katika michuano ya msimu ujao.
Lakini “kapu la watenda madhambi” halitatumika katika fainali za Mataifa ya Ulaya Juni mwaka huu au kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya rais wa Uefa, Aleksander Ceferin, kuiambia Telegraph Sport mwezi uliopita kwamba aliupinga kabisa utaratibu huo mpya, akiongeza: “Hili sasa sio soka tena.”
Hata hivyo Uefa italazimishwa kuutumia utaratibu huo mpya kwa sababu majaribio yatafuatiwa na kujumuishwa kwa utaratibu huo kwenye sheria za soka.
Ozil Aionya Atletico
Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Arsenal amesema kadi hii inaweza kuwaathiri Zaidi Atletico Madrid wanaoshiriki Ligi Kuu ya Hispania, la Liga kwa kuwa ndiyo mafundi wa kuwazonga waamuzi
Atletico wawe makini sana, hii kadi inaweza kuwa shida Zaidi kwao kwa kuwa wanatabia sana ya kugomea maamuzi ya mwamuzi