Kaze amtupa Jukwaani Lamine, Makapu aanza

Yanga inashuka uwanjani saa 10:00 jioni leo Machi 7 na katika kikosi chao Kocha wao Cedric Kaze amefanya mabadiliko manne huku akimtupa jukwaani nahodha wake wa kwanza Lamine Moro.

Katika ukuta wake Kaze amefanya mabadiliko mawili akimrudisha kipa Metacha Mnata lakini pia akimpa nafasi Said Juma akichukua nafasi ya Lamine atakayecheza sambamba na Bakari Mwamnyeto ambaye leo ndio atakuwa nahodha mkuu huku mabeki wengine wakiendelea kuwa Kibwana Shomari kulia na kushoto Yassin Mustapha.

Katika kiungo Kaze amefanya badiliko moja  akimuanzisha Haruna Niyonzima anayechukua nafasi ya Farid Mussa ambaye naye atakuwa jukwaani.

Niyonzima atakuwa sambamba na Mukoko Tonombe,Feisal Salum lakini pia winga Tuisila Kisinda ambaye ndiye aliyefunga bao pekee katika mchezo uliopita wakipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga pia itakuwa na jina moja jipya Ditram Nchimbi akirejea baada ya kukosa mchezo uliopita kufuatia kuwa majeruhi akichukua nafasi ya Michael Sarpong ambaye ameumia na sasa Nchimbi atacheza sambamba na Fiston Abdulrazack.

Kwenye benchi Kaze amewapa nafasi ya kusubiri kipa Farouk Shikhalo,Paul Godfrey,Abdallah Haji,Zawadi Mauya,Deuse Kaseke,Waziri Junior na Yacouba Sogne.