Kumbe Kaizer waliongeza mzigo kwa Miquissone

Wednesday August 04 2021
kaizeripic
By Charity James
By Olipa Assa

KAIZER Chiefs waliongeza dau kwa mzigo Simba, ili kumpata  Luis Miqussone aliyeko kwenye hatua za mwisho kutimkia Al Ahly.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ndani ya Simba ni kwamba, Kaizer Chiefs walionyesha nia ya kuweka mezani Sh 1.5 Bil ikiwa imezidi ile Bil 1 ya Al Ahly ya Misri.

Lakini Mwanaspoti linajua kwamba Luis amewaambia marafiki zake wa karibu ndani ya Simba kwamba anakwenda Al Ahly.

Hadi jana Uongozi wa Ahly ulikamilisha rasmi uhamisho wa winga huyo kutoka Simba kwa ada ya Dola 900,000

Usajili wa winga huyo umekamilika  baada ya kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo

Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara 10 walifikia makubaliano na Simba tangu wiki iliyopita na kilichobakia ilikuwa ni kumalizana na mchezaji huyo.

Advertisement
Advertisement