Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lawi aanzishwa dhidi ya Mashujaa

Muktasari:

  • Coastal ni timu mwenyeji wa mchezo huo unaopigwa ukiwa ni pili kwa timu hiyo na wa tatu wa Mashujaa tangu msimu huu uanze.

Dar es Salaam. Hatimaye beki Lameck Lawi ameibuka kwenye kikosi ya Coastal Union kinachotarajia kushuka dimbani kukabiliana na Mashujaa katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Coastal ni timu mwenyeji wa mchezo huo unaopigwa ukiwa ni pili kwa timu hiyo na wa tatu wa Mashujaa tangu msimu huu uanze.

Lawi ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisubiri hatma ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kutokana na kuhusishwa na kusaini mkataba na Simba ameibuka katika kikosi cha timu hiyo aliyoisaidia msimu uliopita kumaliza nafasi ya nne na kukata tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lawi aliyekuwa ametimkia Gent A.A.K kwa ajili ya kumalizana na timu hiyo ili aitumikie msimu huu alirejea nchini na kushindwa kucheza mechi mbili za kwanza za Coastal Union akisubiri hatma yake.

Leo katika orodha ya majina ya wachezaji 11 wa kikosi kinachotarajia kucheza na Mashujaa jina la Lawi  lipo sambamba na kipa Ley Matampi, Jackson Shiga, Miraji Adamu, Mukrim Issa, Anguti Luis.

Wengine ni Abdallah Hassan, Lucas Kikoti, John Makwattar, Mbaraka Yusuph na Hernest Briyock Malonga.

Katika mechi ya kwanza ya ligi msimu huu, Coastal ililazimishwa sare ya 1-1 na KMC wakati  Mashujaa ilianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kisha kulazishwa suluhu na Pamba.