Lowassa kutinga uwanja wa Taifa kesho

Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa

Muktasari:

"Kesho nakwenda  uwanjani, usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri utaniona  uwanjani" amesema Lowassa ambaye hajawai kuweka wazi ni mshabiki wa timu gani, zaidi ya kusema anaipenda Manchester United.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kesho (Jumamosi) atakuwa miongoni mwa maelfu ya washabiki watakaoudhuria mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayochezwa uwanja wa Taifa jijini hapa.

"Kesho nakwenda  uwanjani, usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri utaniona  uwanjani" amesema Lowassa ambaye hajawahi kuweka wazi ni mshabiki wa timu gani, zaidi ya kusema anaipenda Manchester United.
Lowassa amesema kinachomsukuma zaidi kwenda uwanjani ni kuungana na wadau wa soka nchini na kujionea ambavyo ligi ya Tanzania inavyokuwa na msisimko kama ilivyo kwa ligi za nje.
"Nasikitika ninapoona watu tunazipenda sana timu za nje.Yale mahaba ya zamani kwa timu zetu yako wapi?michezo hususani mpira ni eneo pana sana la ajira kwa vijana wetu," amesema Lowassa ambaye alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu hapo zamani.