Magori: Tukifanikiwa tutaongoza kundi

Khartoum. Mshauri wa benchi la ufundi la Simba, Crescentius Magori amesema kama Simba itafanikiwa kuwafunga Al Marrikh katika mechi ya leo Unakwenda kuweka rekodi ya kumaliza nafasi ya kwanza katika kundi 'A'.

Magori alisema wachezaji wao kama wakifanikiwa kupambana na kupata pointi tatu dhidi ya Al Marrikh maana yake watakuwa wamefikisha pointi tisa katika kileleni cha msimamo wa kundi.

"Tukiwa kileleni mwa msimamo wa kundi tutabakiwa na mechi tatu ambazo mbili tutacheza nyumbani na moja ya mwisho tutakuwa ugenini dhidi ya Al Ahly.

"Ili kufikia malengo ya kumaliza kundi kama vinara tunaenda kucheza na Al Marrikh, ambao kama tumeweza kuwafunga kwao tunashindwa vipi nyumbani kwetu," alisema.

"Jambo hilo hilo linawezekana kwa AS Vita ambao nao tuliwafunga nyumbani kwetu kwa maana hiyo, tutakuwa tumefikisha pointi 15, ambazo zitatuweka kileleni.

"Hamta yetu ya kumaliza kama vinara wa kundi ipo mikononi mwa Marrikh kama tutawafunga katika mchezo huu ambao tunatambua utakuwa mgumu," alisema Magori.

Katika hatua nyingine Magori alisema jambo hilo la kupata ushindi hapa Sudan linawezekana kwa nyakati tofauti alizokuwa katika uongozi wa mpira wamewahi kishinda hapa.

Magori alisema wamewahi kuja na Simba katika miaka ya nyuma wakashibda lakini hata Taifa Stars alikupa nayo mara mbili hapa walishinda ikiwemo mwaka jana walipopata safari ya kufuzu Chan, baada ya kushinda mabao 2-1.

"Kikubwa wachezaji wetu wanahitajika kuwa na nidhamu ya mchezo muda kwa kucheza kwa pamoja wanaposhambulia na kushambuliwa na jambo letu la kupata ushindi linawezekana," alisema.

"Unajua kumaliza vinara katika kundi moja ambalo wapo Al Ahly si jambo dogo na rahisi ila malengo yetu yapo hivyo na tunaimani linawezekana hilo.

"Tumeweka mazingira yote sawa kwa wachezaji ili kufikilia zaidi mechi kuliko jambo lingine lolote, kuhusu changamoto za nje ya uwanja kwa kiasi kikubwa zote tumedhibiti," alisema Magori ambaye ndio alikuwa mkuu wa msafara kutokea Dar es Salaam mpaka hapa Sudan.