Man City yasaka vinne, Man U kumchafulia Tuchel

Muktasari:

  • Manchester City imeelekeza macho yake katika kutwaa vikombe vinne vikubwa wakati vinara hao wa Ligi Kuu ya England wakijiandaa kuivaa West Ham, ambayo kwa sasa ni moto katika mechi za mwishoni mwa wiki hii.
  • Ili kuwa na nafasi ya kuiweka City matatani, Manchester United inayoshika nafasi ya pili katika msimamo huo wa ligi ya soka, itatakiwa imtibulie Thomas Tuchel ambaye tangu aichukue Chelsea hajawahi kupoteza mchezo.

London, England (AFP). Manchester City imeelekeza macho yake katika kutwaa vikombe vinne vikubwa wakati vinara hao wa Ligi Kuu ya England wakijiandaa kuivaa West Ham, ambayo kwa sasa ni moto katika mechi za mwishoni mwa wiki hii.
Ili kuwa na nafasi ya kuiweka City matatani, Manchester United inayoshika nafasi ya pili katika msimamo huo wa ligi ya soka, itatakiwa imtibulie Thomas Tuchel ambaye tangu aichukue Chelsea hajawahi kupoteza mchezo.

Man City kunyoosha misuli
Safari ya Manchester City kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu haikuwa ya kushangaza kutokana na sifa yake ya kutwaa ubingwa, lakini mwenendo huo ulioambatana na kuvunja rekodi umeamsha imani kuwa wanaweza kufikia mafanikio makubwa.


City ilipata ushindi katika mechi ya 19 mfululizo katika mashindano tofauti -- ambayo ni rekodi kwa klabu za ligi ya juu nchini England -- wakati ilipopata ushindi rahisi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Timu hiyo, inayofundishwa na Pep Guardiola na inayoongoza kwa tofauti ya pointi kumi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, inakutana na Tottenham katika mechi ya Kombe la Ligi na imeshaingia robo fainali ya Kombe la FA.
Bernardo Silva, ambaye alikuwa mmoja wa wafungaji dhidi ya Borussia, alizungumzia kujiamini huko kwa City wakati ikikaribia kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kutwaa vikombe vinne.
Ikiwa haijapoteza mchezo katika mechi 26 ilizocheza tangu Novemba, Silva alisema City inaweza kuweka viwango vipya vya mafanikio baada ya kutwaa vikombe vitatu vya mashindano ya ndani misimu iliyopita.
"Tunajua tuna mwenendo mzuri, lakini hii ni hatua tu ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa," alisema. "Tuna Ligi Kuu, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
"Utakuwa msimu mgumu lakini tutatwaa mataji yote."

Man Utd yakabili mtihani wa Tuchel
Manchester United inaipumulia Manchester City kileleni, lakini vijana wa Ole Gunnar Solskjaer watahitaji wapinzani wao waparaganyike ili watwae ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013.
Ushindi dhidi ya Chelsea Jumapili ni muhimu kuweka hai matumaini finyu ya kutwaa ubingwa.
Hiyo haitakuwa rahisi ukitilia maanani kufufuka kwa Chelsea chini ya kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain, Thomas Tuchel.


Tangu ambadili Frank Lampard aliyetimuliwa Januari, Tuchel imeshinda mechi sita kati ya nane za mashindano tofauti na kuipandisha Chelsea hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi.
Lakini United haijashindwa katika mechi tano na mshambuliaji wake, Marcus Rashford anaamini kuwa timu hiyo sasa ni tishio.
"Nadhani tumekuwa tukisema misimu yote kuwa timu hii inakuw abora, tukijifunza katika kila mechi," alisema Rashford.
"Lazima tujiangalie na kuendelea kufanya kilicho bora. Hatimaye hilo litatufanya tushinde mechi."

Dele Alli aibuka
Baada ya kuwekwa nje muda mwingi na kocha Jose Mourinho, mshambuliaji Dele Alli amerejea katika kiwango chake na hivyo kumpa wakati mgumu kocha wa Tottenham katika kupanga timu.
Alli alionekana kukaribia kuondoka kwa mkopo mwezi uliopita kabla ya klabu hiyo kuripotiwa kuzuia jaribio la mchezaji huyo kurudi na kocha wake wa zamani, Mauricio Pochettino katika klabu ya PSG.
Tangu wakati huo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amefanya mazungumzo ya kumaliza tatizo hilo na Mourinho na ameanza kurejeshwa kikosini.


Alli alitumia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wolfsberger Jumatano katika mechi ya Kombe la Europa kudhihirisha ubora wake, akifunga kwa tik-tak na kutoa pasi za mabao mawili.
Tottenham, katika nafasi ya tisa, iliishinda Burnley Jumapili iliyopita na kurudi katika nafasi nne za juu.
"Haya ni mambo yanayoumiza kichwa ambayo nayapenda," alisema Mourinho akimaanisha kuwa na wakati mgumu kupanga kikosi. "Matatizo usiyotaka ni pale wastu wengi wanapokuwa hawafanyi vizuri. Mashaka mengi, na sababu hasi.

Ratiba:
Jumamosi
Manchester City    v West Ham    (saa 6:30)
West Brom    v Brighton    (saa 9:00)
Leeds        v Aston Villa    (saa 11:30)
Newcastle    v Wolves    (saa  2:00)

Jumapili
Crystal Palace    v Fulham    (saa 6:00)
Leicester    v Arsenal    (saa 6:00)
Tottenham    v Burnley    (saa 8:00)
Chelsea        v Man United    (saa 10:30)
Sheffield Utd    v Liverpool    (saa 1:15)

Msimamo
Man City    25 18 5 2 50 15 59
Man Utd        25 14 7 4 53 32 49
Leicester    25 15 4 6 44 27 49
West Ham    25 13 6 6 39 29 45
Chelsea        25 12 7 6 41 25 43
Liverpool    25 11 7 7 45 34 40
Everton        24 12 4 8 35 35 40
Aston Villa    23 11 3 9 37 26 36
Tottenham    24 10 6 8 37 27 36
Leeds        25 11 2 12 43 43 35
Arsenal        25 10 4 11 31 26 34
Wolves        25 9 6 10 26 32 33
Crystal Palace    25 9 5 11 29 43 32
Southampton    25 8 6 11 31 43 30
Burnley        25 7 7 11 18 30 28
Brighton    25 5 11 9 26 32 26
Newcastle    25 7 4 14 26 43 25
Fulham        25 4 10 11 21 32 22
West Brom    25 2 8 15 19 55 14
Sheffield Utd    25 3 2 20 15 41 11