Mashabiki, Simba Yanga nusu wazichape

NJE ya uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ambao utapigwa mechi ya fainali ya kombe la Azam (ASFC) kati ya Simba na Yanga kuanzia saa 10:00 jioni kidogo mashabiki wa timu hizo mbili wapigane wakiwania kuingia uwanjani.

Mrafaruku huo ikiwemo kusukumana na kutoleana maneno machafu umetokea dakika chache kabla ya mageti ya uwanja hup kufunguliwa saa 4:00 asubuhi.

Ilikua kwenye geti namba tano ambapo mashabiki hapo walikuwa wamekusanyika mchanganyiko na baadae mamlaka zikamulu kuwa mashabiki wa Yanga wanahitaji kuingilia geti jingine.

Ubishi kwa timu zote mbili ulianzia hapo na kuleteana ubabe kwa kuvimbiana ambapo baadae walielewana na Yanga kuanza kuchomoka mmoja mmoja wakielekea kwenye geti walilopaswa kuwepo.

Yote hayo ni kuelekea saa 10:00 jioni kwenye mtanange unaotarajiwa kuwa ba mvuto wa aina yake kutokana na historia na tamaduni za timu hizo pale zinapokutana.


MAGETI YAFUNGULIWA

Saa 4:00 asubuhi ndio muda ambao mageti ya uwanja wa Lake Tanganyika yalifunguliwa na kuruhusu mashabiki wente tiketi kuingia ndani.

Kuanzia saa 12:00 asubuhi umati mkubwa wa mashabiki ulijitokeza  nje ya uwanja huo ambapo walipanga foleni zaidi ya tano katika mageti ya uwanjani hapo wakisubili kuingia ndani.

Baada ya mageti kufunguliwa, ilishuhudiwa kila shabiki anayeingia ndani ya uwanja huo akipewa barakoa na kupakwa vitakasa mikono.

Hadi sasa bado mashabiki wanaendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo huku wakitambiana kila mmoja akisifia timu yake.

Mashabiki hao sio wakazi wa mkoani Kigoma pekee, bali wapo wengi kutoka nje ya mkoa huo na wengine wanetoka nchi burundi za Burundi, Congo na Rwanda.

Hii ni mara ya kwanza kwa mkoa wa Kigoma kuhodhi mchezo mkubwa wa namna hii unaowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba timu ambazo zina mashabiki wengi zaidi nchini.