Mo Dewji: Chama yupo Simba hadi 2022

Sunday November 15 2020

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji amesema kiungo, Clatous Chama amesaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo hadi 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 15, 2020, Dewji amesema baada ya kuwepo maneno mengi kuhusiana na nyota huyo kuhusishwa kwenda Yanga wameamua kumuongezea mkataba.

"Ukweli ni kuwa Chama tumeshaini nae mkataba atabaki na Simba hadi msimu wa 2022 kwahiyo ana msimu nusu na miaka miwili imebaki, mimi kama Mwenyekiti siwezi kuja hapa kuongea mambo ya uongo," amesema Dewji

Chama ambaye yupo nchi kwao Zambia leo asubuhi aliandika kwenye mtandao wake maneno yakiashiria kuendelea kusalia klabuni hapo.


Advertisement