Mziki wa Simba kwa Banda

LIGI Kuu Bara imetajwa kama moja ya Ligi Bora kwa Afrika Mashariki na Kati na hilo limemuibua beki wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda akisema mziki wa Simba ukichagizwa na uwekezaji wa bilionea Mohammed Dewji, umechangia jambo hilo na kuziamsha hata timu nyingine.

Beki huyo aliyekuwa akikipiga Highland Park ya Afrika Kusini, alisema uwekezaji wa Mo umeifanya Simba iwe bora na kuchangia ubora wa Ligi Kuu Bara kutokana na makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na klabu hiyo ambayo aliichezea miaka saba iliyopita kabla ya kwenda Baroka FC.

“Kufanya vizuri kwa Simba ni kutokana na uwekezaji ambao umefanywa kwenye klabu hiyo na Mo, amekuwa akipambana kwa nafasi yake kuhakikisha wanapiga hatua,” alisema.