Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota ambao hawajafunga bao Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitaanza rasmi Juni 11 hadi Julai 19 mwaka huu huko Mexico, Canada na Marekani.

Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 kuanza huko Marekani, Canada na Mexico, wapo baadhi ya nyota ambao hawajawahi kucheka na nyavu katika mashindano hayo makubwa duniani.

Baadhi ya nyota hao wapo ambao tayari walishatundika daruga na wengine bado wanaendelea kucheza wakifukuzia kuifuta rekodi hiyo.


Ousmane Dembele

Nyota huyu wa Ufaransa tayari ameshiriki katika Fainali mbili za Kombe la Dunia lakini hajafanikiwa kutikisa nyavu katika michuano hiyo mikubwa duniani.

Mshambuliaji huyu wa PSG alianza kucheza kwa mara ya kwanza katika Fainali za 2018 ambapo Ufaransa ilitwaa ubingwa huo kule Russia kabla ya kuupoteza katika Fainali za 2022 ilipochapwa na Argentina kwa mikwaju ya penalti.

Fainali za mwaka huu zinakua za tatu kwa Dembele ambaye anaonekana kuwa na kiwango bora tofauti na awali, huku akiwa na kibarua cha kuandika bao la kwanza la Kombe la Dunia.


Zlatan Ibrahimović

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Sweden licha ya kuwa ndiye kinara wa ufungaji katika timu hiyo lakini hakuwahi kupata bao katika Fainali za Kombe la Dunia alizoshiriki.

Ibrahimović aliifungia Sweden jumla ya mabao 62 katika maisha yake ya soka, lakini alishindwa kufanya hivyo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la 2002 na 2006 huku akicheza jumla ya mechi tano katika michuano yote miwili.

Nyota huyu wa zamani wa Barcelona, Manchester United na AC Milan alistaafu kucheza soka, Juni 4, 2023 alipokuwa na umri wa miaka 41.


Sergio Ramos

Beki huyu wa zamani wa Hispania alifunga jumla ya mabao 23 katika timu yake ya Taifa, Ramos alicheza katika fainali nne tofauti za Kombe la Dunia lakini hakuwahi kutikisa nyavu za wapinzani wake.

Licha ya kukosa bao katika Fainali za Kombe la Dunia, beki huyo alitoa mchango mkubwa akiisaidia Hispania kushinda taji hilo katika Fainali za 2010 zilizofanyika Afrika Kusini.


Luís Figo

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Ureno alishiriki katika Fainali mbili za Kombe la Dunia lakini hakufanikiwa kuandika bao kwenye fainali za 2002 na 2006.

Licha ya kuifikisha Ureno katika hatua ya nusu fainali za 2006 zilizofanyika Ujerumani, nyota huyo bado alishindwa kufumania vyavu katika mashindano hayo makubwa duniani akicheza jumla ya mechi 10.


Frank Lampard

Iwapo bao alilofunga katika Fainali za 2010 lingekubaliwa huenda kiungo huyo wa zamani wa England hasingekuwa katika orodhaa hii ya mastaa ambao hajawahi kuandika bao katika michuano hiyo mikubwa duniani.

Katika mechi ya robo fainali dhidi ya Ujerumani, Lampard aliachia shuti kali lililomshinda kipa, Manuel Neuer ambapo mpira huo ulidunda ndani ya lango na kurudi uwanjani huku refa akiendelea na mchezo.

Baada ya hapo aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter alijitokeza na kuomba radhi huku akiahidi kuleta teknolojia itayosaidia kurejea matukio ya mpira ulioingia ndani na kurudi uwanjani (Goal Line Technology).