Pele: Marta ni zaidi ya mwanasoka

Thursday July 22 2021
Pele pc

Rio de Janeiro, Brazil. Gwiji wa soka wa Brazil, Pele amemsifu mchezaji wa timu ya wanawake ya nchi hiyo, Marta akisema kuwa "ni zaidi ya mwanasoka" baada ya kufunga katika mechi ya Michezo ya Olimpiki ambayo anashiriki kwa mara ya tano.


Kiungo huyo mwenye miaka 35 alifunga mabao mawili wakati Brazil ilipoanza kampeni yake katika Michedzo ya Olimpiki jijini Tokyo kwa kuirarua China kwa mabao 5-0.


"Natumaini unaota kuhusu kile ulichofanya saa chache zilizopita. Kuzungumzia ni kitu gani, ni ndoto ngapi unadhani ulihamasisha (watu) leo?" Pele ameandika katika akaunti yake ya Instagram.
"Mafanikio yake yana maana kubwa zaidi ya rekodi yako binafsi.

Wakati huu unahamasisha mamilioni ya wanamichezo kutoka michezo mingine, kutoka duniani kote, ambao wanataka watambulike.


"Hongera. Hongera, wewe ni zaidi ya mchezaji wa mpira wa miguu. Unasaidia kujenga dunia nzuri zaidi kutokana na kipaji chako (katika mchezo), ambao wanawake wanapata nafasi zaidi."


Pele alitwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Brazil mwaka 1958, 1962 na 1970.

Advertisement


Kama Pele, Marta anavaa jezi ya timu ya taifa ya nchi yake yenye namba 10 ambayo inapendwa na wengi.

Advertisement