Presha ya majibu ya corona yawakera mabosi Yanga

Kama kuna kitu kinasubiriwa na hamu katika kambi ya Yanga ni kujulikana kwa majibu ya vipimo vya Uviko 19 (Covid 19).

Msafara mzima wa Yanga na wadau wengine ulifanya vipimo vya Uviko 19 jana saa 11 asubuhi kama ambavyo kanuni ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika CAF inavyoelekeza.

Hata hivyo wakati majibu hayo yakisubiriwa presha kubwa imeonekana kuwakumba vigogo wa Yanga wakipokea taarifa za uvumi kutoka kwa wenzao wa Tanzania.

Hatua hiyo imeonekana kuwakera mabosi wa Yanga wakionekana kuchukukizwa na hatua hiyo inayodai wachezaji wao idadi tofauti kuwa wamekutwa na maambukizi.

Hata hivyo wakiwa katika ukumbi wa chakula wachezaji wenyewe wameonekana wachangamfu wakati wa kupata kifungua kinywa.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema bado hawajapokea majibu hayo lakini wakati wowote yatafika.

Senzo ameongeza hata wao wanayasubiri kwa hamu majibu hayo akiwataka mashabiki wa Yanga kutoyumbishwa na uvumi huo badala yake waombee taarifa njema.

"Sisi huku ndio tumechukuliwa vipimo na hata sisi tunahamu ya kujua majibu mashabiki na wanachama watulie majibu yatatoka na tunatarajia taarifa njema," amesema Senzo ambaye alitangulia nchini hapa.

"Tunajua kuna watu wanaombea majibu yawe mabaya kitu muhimu kwa watu wetu wa Yanga ni kutoyumbishwa na taarifa hizo wao wanatakiwa kutuombea mambo yawe mazuri.