PSG yamtema Phil Collins, sasa yamtumia DJ Snake

PSG yamtema Phil Collins, sasa yamtumia DJ Snake

Muktasari:

  • Klabu ya Paris Saint-Germain imeachana na wimbo wa Phil Collins unaotumiwa wakati wachezaji wake wakiingia uwanjani na sasa inatumia wimbo wa mtayarishaji DJDJ Snake, ambaye hata hivyo hajafurahia.
     


Paris, Ufaransa (AFP). Klabu ya Paris Saint-Germain imeachana na wimbo wa Phil Collins unaotumiwa wakati wachezaji wake wakiingia uwanjani na sasa inatumia wimbo wa mtayarishaji DJDJ Snake, ambaye hata hivyo hajafurahia.
"Niliwapa sauti kwa ajili ya hafla ya kumtambulisha Lionel Messi" kwenye uwanja wa Parc des Princes, ameandika mtayarishaji muziki huyo ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa na ambaye amefanya kazi na Lady Gaga na ametajwa kuwania tuzo za Grammys.  


"Nimegundua kuwa sasa unatumiwa kwa ajili ya wachezaji kuingia uwanjani wakati haufai," ameandika.
Kabla ya kuifunga Clermont Jumamosi, wimbo wa "Who Said I Would" ulioimbwa na Phil Collins, ambao umekuwa ukitumiwa kwenye uwanja huo wa klabu ya PSG tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini, haukutumiwa na badala yake uliwekwa wimbo wa DJ Snake wakati wachezaji wakitoka vyumbani.
Lilikuwa ni badiliko lililowazuzua baadhi ya mashabiki, hasa kwenye mitandao ya kijamii, akiwemo shabiki mwenyewe wa PSG, DJ Snake.
Alisema hakutaka kuivuruga klabu kwa "kuzungumzia hadharani suala hili, lakini siwezi kukubali hali hii kama shabiki".