Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rasmi Yanga yahama Chamazi, yaifuata Simba

Muktasari:

  • Yanga imecheza mechi tano za Ligi Kuu msimu huu katika Uwanja wa Azam Complex, ikipata ushindi mara tatu na kupoteza mechi mbili.

Dar es Salaam. Yanga SC imetangaza rasmi kuanza kutumia Uwanja wa KMC Complex kama Uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi za mashindano ya ndani zilizosalia msimu huu.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga kupitia ofisi ya Afisa Mtendaji Mkuu, imesema kikosi chao kitatumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za Ligi Kuu Bara na zile za Kombe la Shirikisho la CRDB.

Aidha imesema kwa mechi zingine za mashindano kama zitaruhusiwa kutumika kwenye Uwanja huo zitachezwa kwenye Uwanja huo.

Kabla ya maamuzi hayo Yanga ilikuwa unatumia Uwanja wa Azam Complex kama Uwanja wao wa nyumbani kwa mechi za Ligi, Kombe la CRDB na hata zile za mashindano za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hata hivyo, Yanga haikueleza sababu za kuukimbia Uwanja wa Azam Complex ingawa Mwananchi Digital inafahamu kuwa Kuna baadhi ya taratibu za kiuendeshaji ambazo mabosi wa Yanga wamedai kukerwa na wamiliki wa Uwanja huo.

Kuhamia Uwanja wa KMC Complex kutaifanya Yanga kuifuata timu yao ya Soka ya Wanawake, Yanga Princess na watani wao Simba ambao wamekuwa wakitumia Uwanja huo.

Uwanja huo pia unatumiwa na timu ya KMC.