Simba yavuta mtambo wa mabao

Wednesday August 04 2021
simba mtambopic
By Charity James

KINARA wa mabao wa Kagera Sugar, Yusuf Mhilu ni miongoni mwa nyota watakao vaa jezi za Simba msimu ujao baada ya kutangazwa na mabingwa hao mfululizo wa Ligi kuu.

Mhilu amejiunga na Simba akitokea Kagera Sugar ambapo aliifungia timu yake mabao tisa msimu uliomalizika.

Nyota huyo anaungana na Winga Peter Banda ambaye ametambulishwa jana baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Mshambuliaji huyo ameonyesha ukomavu baada ya kuachwa na Yanga hakukata tamaa alipambana kupata nasafi ya kuitumikia Ndanda ambako alicheza msimu mmoja tu.

Baada ya kumalizana na Ndanda ambayo ilishuka daraja alipata nafasi nyingine Kagera Sugar ambako ameonyesha uwezo wa  juu na kuwashawishi matajiri wa Simba ambao wameamua kumpa mkataba .

Advertisement