Taifa Stars, Malawi ngoma ngumu dakika 45

Dakika 45, za kwanza za mechi ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania na Malawi zimemalizika kwa suluhu kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo ulianza kwa timu zote mbili kucheza kwa nidhamu kubwa huku Stars ikionekana kushambulia zaidi kwa dakika za mwanzoni.

Dakika ya nne Mhilu alipiga kiki iliyoenda nje baada ya kupigiwa pasi mpenyezo na Mudathir Yahya.


Pia dakika  ya nane Stars walitengeneza shambulizi lingine kupitia upande wa kulia kwa Shomari Kapombe aliyepiga pasi ya chini chini kwenye eneo la boksi la 18 la Malawi na kuwapita washambuliaji bila kuugusa mpira.

Kadri muda ulivyozidi kusogea, Stars waliendelea kutengeza mashambulizi mara kwa mara yakini hayakuzaa matunda.

Malawi walipata kona dakika ya 17 baada ya kufanya shambulizi la kushitukiza kwenye lango la Stars lakini haikuwa na faida kwao kwani iliondoshwa kaenye eneo la Stars na Feisal Salum.

Baada ya hapo Malawi walianza kufunguka na kutafuta bao na kuwafanya Stars kuanza kucheza kwa tahadhati zaidi hususani eneo la ulinzi na kiungo.

Dakika ya 25 mchezaji wa Malawi Mhango Gabaduhwo alionesha kadi ya njano baada ya kuonekana kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi ya kutoa adhabu ya faulo kwa timu yao baada ya Yusuph Mhilu kuangushwa pembeni kidogo ya boksi la 18.

Dakika ya 37 hadi 39 lango la Stars lilikuwa kwenye hatari baada ya Malawi kutengeneza mashambulizi matatu yakiwemo mawili ya mipira ya kona lakini hayakuzaa matunda kwao.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu iliyokuwa imepata bao.