Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tebogo, mwanariadha aliyeipa heshima Afrika

Muktasari:

Majina yaliyokuwa yakitajwa sana ni Wamarekani Noah Lyles na Kenny Bednarek kutokana na kile walichowahi kukifanya katika mashindano tofauti hapo nyuma lakini pia historia isiyovutia ya Waafrika kwenye mbio hizo katika michezo ya Olimpiki.

Letsile Tebogo hakuwa ni mkimbiaji aliyepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi wa mbio za mita 200 katika michezo ya Olimpiki iliyomalizika jana huko Ufaransa.

Majina yaliyokuwa yakitajwa sana ni Wamarekani Noah Lyles na Kenny Bednarek kutokana na kile walichowahi kukifanya katika mashindano tofauti hapo nyuma lakini pia historia isiyovutia ya Waafrika kwenye mbio hizo katika michezo ya Olimpiki.

Hata hivyo Alhamisi, Agosti 8, Tebogo aliishtua dunia baada ya kuwaacha kwenye mataa Bednarek na Lyles na kutwaa medali ya dhahabu kufuatia ushindi alioupata kwenye mbio za mita 200 huku Bednarek akimaliza katika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Lyles.

Tebogo aliibuka mshindi baada ya kukimbia kwa muda wa sekunde 19:46 ambao ulitosha kumfanya avunje rekodi ya kutumia muda mfupi zaidi wa mita 200 ya Afrika iliyoshikiliwa kwa muda wa miaka 28 na Frankie Fredericks wa Namibia ambaye alitumia muda wa sekunde 19:92 mwaka 1996 katika mbio za Meeting Pas de Calais, jijini Paris Ufaransa.

Lakini aliandika historia ya kuipa Botswana medali ya kwanza ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki  huku pia akiweka rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mbio za mita 200.

Heshima kwa mama

Tebogo anasema kuwa ameamua kutunuku ushindi huo wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 olimpiki kwa marehemu mama yake Seratiwa Tebogo ambaye kwa sasa ametangulia mbele za haki.

Mkimbiaji huyo anasema kuwa mama yake mzazi huyo ambaye alifariki mwezi Mei mwaka huu alikuwa akimpa sapoti kubwa katika ushiriki wake kwenye mashindano tofauti na anatamani angekuwepo kushuhudia akitimza ndoto za kushinda medali ya dhahabu Olimpiki.

“Ni kama kimsingi nimembeba yeye katika kila medali ninayopata uwanjani. Anatazama huko aliko na ana furaha sana. Sitaki kuweka tarehe ya kifo chake kwa sababu nitajisikia vibaya.

“Ilikuwa mbio nzuri sana kwangu. Tulipoingia fainali, kocha wangu aliniambia kazi yangu imekwisha sasa ni jukumu lako kuona nini utafanya. Iwe umepata medali au hujapata, maliza mbio ukiwa na afya. Nina furaha nimemaliza mbio nikiwa na afya tele zaidi ya mwanzo,” alisema Tebogo.

Afunga na mbio za vijiti

Kama unadhani Tebogo alibahatisha kupata ushindi kwenye mbio za mita 200 basi unajidanganya kwani hakuishia hapo tu.

Mwanariadha huyo siku mbili baada ya kupata ushindi katika mita 200, aliiongoza timu ya Botswana kuibuka mshindi wa pili katika mbio za Mita 4x 400 kupokezana vijiti, ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Marekani na Uingereza ilishika nafasi ya tatu.

Ni mshindi toka zamani

Medali ya dhahabu kwenye Olimpiki Mita 200 wanaume haikuwa ya kwanza kwa Tebogo kwani kabla ya hapo ameshawahi kunyakua katika mashindano mengine tofauti.

Nyota yake ilianza kung’aa mwaka 2021 alipoibuka mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za dunia mita 100 kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21.

Alikuja kushinda tena medali hiyo katika mashindano kama hayo kwa mwaka uliofuata na mwaka 2022 akawa bingwa wa Afrika kwa wanaume mbio za mita 200.

Medali ya mwisho ya dhahabu kwa Tebogo kushinda kabla ya Olimpiki ni ya Mbio za dunia kupokezana vijiti mwaka 2024 huko Nassau Bahamas.

Mbali ya hizo, ana medali nne za shaba za mashindano tofaufi na pia ana medali moja ya fedha.

Umri unaruhusu

Inawezekana Tebogo akapata mafanikio makubwa zaidi katika mashindano mbalimbali siku za usoni kutokana na umri wake kuwa mdogo.

Tebogo ana umri wa miaka 21 akiwa amezaliwa Juni 7, 2003, akiwa na urefu wa mita 1.84 huku