Ujio wa Kaze wamrejesha nyota Yanga

Ujio wa Kaze wamrejesha nyota Yanga

Muktasari:

  • BENCHI la ufundi la klabu ya Yanga limeshauriwa kuwa kitu kimoja na kukubaliana katika majukumu yao ili waweze kuzalisha kitu kizuri kupitia wao.

BENCHI la ufundi la klabu ya Yanga limeshauriwa kuwa kitu kimoja na kukubaliana katika majukumu yao ili waweze kuzalisha kitu kizuri kupitia wao.

Mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye ni raia wa Burundi Fiston Abdulazaq anayekipiga Uarabuni kwa sasa ameiambia Mwanaspoti kuwa, urejeo wa Cedrick Kaze ndani ya timu hiyo utakuwa na manufaa na faida kubwa.

Fiston amesema endapo makocha katika benchi la ufundi chini ya Nesreddine Nabi wataelewana na kukubaliana kile ambacho kila mmoja anakisema, Yanga itakuwa bora zaidi ya sasa.

"Ila naamini kama wakielewana na kusikilizana na kukutanisha mawazo yao na kuafikiana Yanga itakuwa ya moto sana, uwezo wa Kaze naujua, hata wachezaji tulikuwa tunamkubali sana,"

"Anajua kujenga umoja kwenye klabu wachezaji tunapendana hata kukaa benchi unakuwa unatabasamu na kufurahi ukiamini muda wowote anakupa nafasi ya kucheza,"amesema Fiston.

Aidha Fiston amesema hakuwahi kuona udhaifu wa Kaze mpaka Yanga walipoamua kumuondoa kikosi japokuwa alikuwa sawa muda wote.

"Kurudi itakuwa mwanzo mzuri wa Yanga kuanza kushinda na kufanya vizuri kabisa lakini kurudi ni jambo moja na kupewa nafasi ya kuonyesha mchango wake ni kitu kingine, karudi nasikia kama kocha msaidizi hapo mwenye kauli ya mwisho ni kocha mkuu,".

Kaze ametua nchini jana usiku tayari kwa kuanza majukumu mapya ndani ya Yanga ikiwa ni miezi sita tangu afungashiwe vilago.