Wasudani wa Yanga CAF kutua Dar Alhamisi

Wapinzani wa Yanga CAF kutua Dar Alhamisi

BAADA ya jana viongozi wa Al Hilal kutua Jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Congo, wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo wanatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi tayari kwaajili ya kuikabili Yanga kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika utakaopingwa jumamosi tarehe 8 mwenzi huu.

Hilal kwa sasa bado ipo DR Congo ikiendelea kujiweka fiti ambapo kwenye ziara yao hiyo nchini humo tayari wameshacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Don Bosco siku ya Jumapili na kushushiwa kipigo cha mabao 3-1, ambapo wachezaji wa Don Bosco walivaa jezi za TP Mazembe katika mchezo huo.

Hata hivyo kikosi hicho leo asubuhi kimeendelea kujifua kikiwa chini ya kocha mkuu Florient Ibenge.

Ikumbukwe mabingwa hao wa Sudan walisonga mbele na kuingia kwenye hatua hii baada ya kuitoa St. George ya Ethiopia kwa bao la ugenini ambapo kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walifungwa mabao 2-1 kisha waliporudi nyumbani wakaibuka na ushindi wa bao 1-0.