Watakaoanza Simba hawa hapa
Muktasari:
Mazoezi ya mwisho ya Simba yamekamilika muda huu katika uwanja wa Al Hilal ya hapa Khartoum Sudan.
SUDAN
Mazoezi ya mwisho ya Simba yamekamilika muda huu katika uwanja wa Al Hilal ya hapa Khartoum Sudan.
Mazoezi hayo ya Simba ambayo yalifanyika kwa saa moja tu, kuanzia saa 8:30 mchana mpaka saa 9:30 mchana kwa saa za hapa Sudan.
Wachezaji wa Simba hawakufanya mazoezi mengi magumu wala kukimbia bali ni yale machache tena mepesi mepesi.
Miongoni mwa mazoezi ambayo walilifanya walikimbia mbio za mwendo wa kawaida na walizunguka uwanja mara mbili, mazoezi ya viungo, utimamu wa akili na mengine machache.
Zoezi la mwisho ambalo Simba walifanya la kucheza timu mbili na hapo Mwanaspoti lilibaini wachezaji ambao wanakwenda kuanza katika kikosi cha kwanza.
Manula/Kakolanya
Katika eneo la makipa Aishi Manula alianza kufanya mazoezi mengi ya kutosha na baada ya muda alipumzika.
Akabaki Benno Kakolanya na Ally Salim wakiendelea na mazoezi kwa maana hiyo ikitokea, Manula hayupo sawa anaweza kuanza Kakolanya.
Shomary Kapombe
Katika eneo la beki wa kulia Kapombe alipewa nafasi ya kuanza na alifanya mazoezi mengi ya kukaba na kuzuia.
Mohammed Hussein
Beki wa kushoto anapewa nafasi ya kuanza na mazoezi yake yalifanana na Kapombe.
Joash Onyango
Alipewa nafasi ya kumkata Meddie Kagere na John Bocco na yupo katika kikosi cha kwanza.
Pascal Wawa
Kama ilivyokuwa kwa Onyango nae alipewa majukumu kama hayo.
Taddeo Lwanga
Ataanza katika cha kwanza katika nafasi ya kiungo mkabaji akimpora namba Jonas Mkude.
Clatous Chama
Anaanza katika kikosi cha kwanza atacheza kama winga wa kulia ila atasaidia zaidi katika eneo la kiungo.
Mzamiru Yassin
Atakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza anaanza kama kiungo mshambuliaji lakini atakuwa akimsaidia Lwanga kukaba.
Chriss Mugalu
Mfungaji wa bao katika mechi ya ugenini dhidi ya As Vita anaanza katika kikosi cha kwanza.
Larry Bwalya
Atakuwa nyuma ya straika kurahisha kupata mipira na kutengeneza mashambulizi ya mara kwa mara.
Luis Miquissone
Mfungaji wa bao katika mechi iliyopita dhidi ya Al Ahly ataanza katika kikosi cha kwanza atakuwa akimsaidia Tshabalala kukaba pia.
Wakati mwingine alionekana Mkenya, Francis Kahata akiingia na kutoka kwenye nafasi hii.