Yanga yabanwa nyumbani

Yanga imeruhusu kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wageni Rivers United ya Nigeria kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Bao la dakika ya 51 la Mosse Omuduemuke lilitosha kuipa Nigeria ushindi wa ugenini katika mchezo huo uliochezwa bila mashabiki.

Emuduomuke alichumpa nakumalizi kwa kicha mpira wa kona baada ya wachezaji wa Rivers kugongea na kumkuta mfungaji aliyechumpa nao kwa kichwa na kujaa wavuni.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa inahitaji ushindi wa mabao kuanzia 2-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Nigeria Septemba 19 ili kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kipa wa Nigeria alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari za wachezaji wa Yanga, Herieter Makambo, Yacouba Songne na Feisal Salum katika mchezo huo ambao kipa wa Yanga,  Djugui Diarra licha ya kufungwa bao hilo, alipangua hatari za wazi langoni mwake dakika ya 45 ba 72.