Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaunda kikosi kazi cha makombe

Muktasari:

  • Yanga hii iliyosumbua ikichukua mataji na kufanya makubwa Afrika, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na Gumbo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mabingwa hao.

Kikosi cha Yanga kwa kundi la pili limepaa leo alifajiri kuifuata CBE SA ya Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kabla ya kung'oa rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said ameunda jeshi jipya la kikosi kazi ambacho kina matajiri na sura za rekodi.

Hersi ameunda kamati mpya ya mashindano yenye watu nane akiendelea kumuamini Rodgers Gumbo aliyerejeshwa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo akiwa na rekodi ya maana.

Yanga hii iliyosumbua ikichukua mataji na kufanya makubwa Afrika, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na Gumbo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mabingwa hao.

Nyuma ya Gumbo amerejeshwa pia Lucas Mashauri atakayeendelea kuwa makamu ambaye alikuwa na mwenyekiti wake ikichukua mataji hayo ya ndani tisa kwa misimu mitatu.

Ndani ya kamati hiyo wamo wajumbe sita wakiwemo watu wazito wawili Seif Ahmed 'Seif Magari' na swahiba wake, Davis Mosha ambao ni vigogo wa muda mrefu ndani ya timu hiyo.

Seif Magari amewahi kuongoza kamati hiyo wakati wa utawala wa Marehemu Yusuf Manji kwa mafanikio makubwa, huku Mosha akiwahi kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa marehemu Imani Madega.

Mbali na wawili hao, wengine ni Pelegrinius Rutayuga, injinia Mustapha Himba, Majid Suleiman wakati sura mpya ikiwa moja ya Omary Kimosa.

Taarifa za ndani ambazo Mwananchi imezinasa kwa uhakika ni kwamba kamati hiyo tayari ilishaanza kazi kimyakimya ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha timu hiyo inakwenda kutetea mataji yote ya ndani lakini pia kuhakikisha Yanga inafika mbali katika Ligi ya Mabingwa.

Nusu ya vigogo hao watashuka nchini Ethiopia kuhakikisha wanaendelea ubabe wao baada ya kuwang'oa Vital'O ya Burundi.


YATUA KWA MAKUNDI

Yanga itatua nchini Ethiopia kwa makundi tofauti ambapo hapa unavyosoma hivi sasa kundi la wachezaji waliokuwa nchini Ivory Coast na kikosi cha Taifa Stars limeshatua nchini humo na kupokelewa kisha baadaye kundi la pili ni lile litakalotoka hapa nchini kisha watafuata kipa Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki na mshambuliaji Prince Dube.

Tayari Yanga ilishawatanguliza watu wawili akiwemo Mkurugenzi wa Mashindano, Ibrahim Mohammed Ethiopia kuandaa taratibu zote za awali.

Yanga itashuka uwanjani keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa kuvaana na CBE kabla ya kurudiana nao wiki ijayo na mshindi wa jumla kutinga makundi, Yanga ikitaka kuandika rekodi ya kufika hatua hiyo kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopita kutinga baada ya miaka 25 kupita na kwenda hadi robo fainali kabla ya kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.