Zoezi la utoaji namba Kili Marathon 2021 kufanyika Arusha

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam waiojitokeza katika viwanja vya Mlimani City kuchukua namba za ushiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 tayari kwa mashindano yatakayofanyika mjini Moshi Jumapili ijayo.

Baada ya mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza katika viwanja vya Mlimani City kuchukua namba zao za ushiriki katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021, zoezi hilo sasa linahamia Arusha Jumanne na Jumatano.

Akizungumza mara baada ya kufunga zoezi la Dar es Salaam, mwakilishi wa kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company, Rajon Datoo alisema zoezi hilo lilikuwa na  mafanikio makubwa kwani wengi waliweza kuchukua namba zao.

“Tumepokea ushirikiano mkubwa kutoka kwa wakazi wa Dar es Salaamambao wamefanya zoezi hili liende haraka,” alisema.

 “Tunawaomba waliojisajili mbio ndefu za Kilimanjaro Premium Lager (kilomita 42), mbio za nusu marathon za kilomita 21 za Tigo na zile za kujifurahisha za kilomita 5 za Grant Malt wafike Kibo Palace Hotel JUmanne Februari 23 na Februari 24 kuanzia saa nane mchana hadi saa moja usiku,’ alisema na kuongeza kuwa washiriki wanaombwa kukumbuka kwenda na vitambulisho na ujumbe wa uthibitisho wa malipo.

Baada ya Arusha zoezi hilolitahamia Moshi kuanzia Februari 25 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 26 (saa nne asubuhi hadi saa mbili usiku) na Februari 27 (saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni).

Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam waiojitokeza katika viwanja vya Mlimani City kuchukua namba za ushiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 tayari kwa mashindano yatakayofanyika mjini Moshi Jumapili ijayo.

Kwa mujibu wa waandaaji, zoezi la uandikishaji kwa ushiriki katika mbio za km 42 na Km 5 bado unaendelea katika vituo vya kutolea namba na

Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager-kwa upande wa mbio ndefu za kilomita 42km, Tigo wamedhamini mbio za kilomita 21km (Half Marathon) wakati Grand Malt wamedhamini mbio za kilomita 5km.

Wadhamini wa vituo vya kunywa maji (water table) ni   Unilever Tanzania, Simba Cement, TPC Sugar, Kilimanjaro International Leather Company Limited, Kibo Palace Hotel na watoa huduma maalumu ni Garda World Security, Keys Hotel na CMC Automobile.

Mbio hizi zimeandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kitaifa zinaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions Limited.