Zolan atetetea mastaa wake

Thursday August 11 2022
zolan pic
By Mwandishi Wetu

Baada ya tamasha la Simba Day juzi Jumatatu, kocha Zoran Maki amesema wachezaji walicheza kwa presha ya juu na kushindwa kufanya alichowaelekeza.

Maki ameliambia Mwanaspoti mastaa wake hawakucheza vizuri tofauti na matarajio, huku akikiri kuwa ni kutokana na presha waliyokuwa nayo kutokana na umati mkubwa uliojitokeza kuwapa sapoti. “Timu ni nzuri lakini imecheza kwa presha.Ukiangalia kila mchezaji aliyepata nafasi ameonyesha kitu, natarajia mambo mazuri zaidi kutoka kwao,” alisema

“Ubora wa mchezaji mmoja mmoja naamini kila mtu ameona kutokana na timu kuchezwa sehemu ya wazi. Kila mmoja alifanya jukumu alilopewa. Bado tunajenga timu imara.”

Kuhusu straika Habibu Kyombo, Maki alisema ni mchezaji mzuri ambaye anaamini anaweza kuwa bora zaidi kwa taifa miaka ya karibuni kama ataendelea na ubora alionao.

“Kyombo ni mchezaji mzuri nitaendelea kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili aonyeshe nachokiona mguuni kwake. Ni namba tisa mzuri ambaye anaweza kucheza vizuri na mabeki pia ana nguvu na kasi,” alisema Maki.

Advertisement