Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa ya chama hicho, Janeth Rithe (kulia) wakiangalia kadi za CCM zilizotoka kwa waliokuwa wanachama wa chama hicho waliojiunga na ACT – Wazalendo wilayani Tanganyika mkoani Katavi jana Agosti 4, 2024. Chama hicho kimedai kupokea kadi za waliokuwa wanachama wa CCM kutoka kaya 800 zinazoishi katika Mtaa wa Luhafwe, wilayani humo. Picha na ACT-Wazalendo