Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe leo Oktoba 1, 2024 amezindua kiwanda cha kubanguwa korosho kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (Tanecu) kilichopo katika Kijiji cha Mmoyo wilayani Newala mkoani Mtwara.
Kiwanda hicho kina uwezo wa kubangua korosho tani 3500 kimejengwa kwa thamani ya Sh3.4 bilioni na kinatarajia kuanza ubanguaji katika msimu wa mwaka 2024 / 2025. Picha na Edwin Mjwahuzi