Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu akizungumza bunge alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadiro ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jijini Dodoma leo. Jesca ameitaka jamii kuwalinda watoto wa kiume ili kutunza mbegu ya kiume ya kitanzania, kutokana na matukio ya kikatili wanayofanyiwa baadhi ya watoto hao ikiwemo kulawitiwa. Picha na Edwin Mjwahuzi