Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kushoto) akipokea kadi za vyama vya upinzani kutoka kwa waliokuwa wanachama wa vyama hivyo waliojiunga CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma Mjini jana Agosti 4, 2024. Jumla ya wapinzani 200 wanakadiriwa kujiunga CCM wakitokea upinzani katika mkutano huo, akiwemo mbunge wa zamani wa viti maalumu (Chadema), Sabrina Sungura. Dk Nchimbi tangu alipoanza ziara zake baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo Januari 2024 ametembelea mikoa 13 na amepokea wanachama wapya zaidi 5,000 kutoka upinzani. Picha na CCM