Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi anaendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo jana Jumapili Agosti 11, 2024 aliingia mkoani Geita akitokea Kagera. Akiwa wilayani Chato alitembelea kaburi la Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Dk John Magufuli na msafara wake ulishiriki sala fupi ya kumuombea kiongozi huyo.
Nchimbi amesema kazi kubwa anayoifanya na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ndiyo namna sahihi ya kumuenzi hayati Magufuli. Na Mpigapicha Maalumu