Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Dk Joseph Mhagama (wa pili kulia) akizungumza leo jijini Dodoma, alipokuwa akiongoza kikao cha kamati hiyo ilipokuwa ikiendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu miswada minne ya sheria iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge. Miswada hiyo ni muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa Mwaka 2023, muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Mwaka 2023, muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria za vyama vya siasa wa Mwaka 2023. Na Mpigapicha Maalumu