Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu amewasili leo Jumatano, Januari 25, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Ubelgiji.
Mamia ya wafuasi wa Chadema wamefurika katika barabara ya kwenda uwanja wa ndege kumlaki kiongozi huyo huku wakiimba na kucheza huku vigoma vikipigwa pamoja na mavuvuzela.