Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo Septemba 11, 2024 amefungua mkutano wa nane wa mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito ulioanza leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Majaliwa amefungua mkutano huo kwa niaba Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amesema mkutano huo utatoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji endelevu wa samaki. Picha na OWM