Simba imedondosha pointi mbili baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine.
Baada ya matokeo hayo Simba inafikisha sare nne kwa msimu huu ikiwa na pointi 28 katika michezo 13 huku ikishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi nyuma ya Azam na Yanga ikiwa kileleni.
Mbeya City inapanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi baada ya michezo 13 ikijikusanyia pointi 19.