Aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya BOA, Tawi la Kahama, Neema (Martha) Towo (30) alizikwa jana Jumatatu nyumbani kwao katika Kijiji cha Mrimbo, Mwika, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Neema alidaiwa kutekwa na kuuawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana Machi 8 mwaka huu Kibaha mkoani Pwani alipoenda kusalimia wazazi wake. Picha na Janeth Joseph