Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango leo Novemba 06, 2024 ameshiriki mazishi ya marehemu John Tutuba ambaye ni Baba mzazi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba yaliyofanyika kijijini kwake Kibondo mkoani Kigoma. Mazishi hayo yametanguliwa na Ibada ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu Wilayani Kibondo na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhashamu Askofu Joseph Mlola. Picha na OMR