Rais Samia Suluhu Hassan amewatembelea na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere wakati alipokwenda nyumbani kwake Msasani, huku akimtembelea pia na kumfariji Mama Dorcas Membe Mjane wa Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Hayati Bernard Membe wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.