Hali ya simanzi na huzuni imetawala wakati wa kuagwa kwa mwili wa Theresia Mdee, mama mzazi wa mbunge wa viti maalumu, Halima Mdee katika ibada ya kumuaga iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kibangu, Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 5, 2024 kabla ya kusafirisha kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko. Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ni miongoni walihudhuria ibada hiyo. Picha zote na Michael Matemanga