Afrika bora kwa watoto: Kwa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania

C-Sema

Tanzania inakadiriwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni duniani. Kwa wastani, karibu wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 na 37% ya wanawake  enye umri wa miaka 20-24 wameolewa ama wako kwenye mahusiano ya kinyumba kabla ya umri wa miaka 18. Taarifa zinathibitisha kushuka kwa 4% tangu mwaka 2004 (Kwa mujibu wa TDHS 2012).

Huduma ya Simu kwa Mtoto hupokea kesi 7 za ndoa za utotoni kila mwezi jambo ambalo limeulazimu uongozi wa Huduma hii kuungana na Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za utotoni (TECMN), ambao ni muungano wa asasi 35 zinazofanya kazi pamoja kutokomeza ndoa za utotoni

Tanzania hususani, kuongeza uelewa wa madhara ya ndoa za utotoni katika ngazi ya jamii na taifa; kushwawishi mabadiliko ya sheria ili kutokomeza ndoa za utotoni; na kutafuta rasilimali kuwawezesha wasichana walioolewa na walio katika hatari ya kuolewa; na kuimarisha na kuratibu taasisi zenye malengo ya kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania.

Save the Children

Utafiti uliofanywa na Save the Children umeonyesha kwamba elimu na makazi salama yasiyo na migogoro ni miongoni mwa masuala yanayosaidia kuwalinda wasichana dhidi ya ndoa za utotoni. Hii inatokana na kwamba kuwatunza wasichana shuleni huchelewesha ndoa za utotoni wakati makazi salama huwazuia wasichana na wavulana kuingia kwenye ndoa za utotoni ili kukwepa adhabu kali. Kuwawezesha wasichana husaidia kuwaongezea kujithamini na kuwapunguzia uwezekano wa hatari ya kushawishiwa na wanaume watu wazima kwa zawadi na pesa.

Ufahamu na uhamasishaji wa Jamii kwamba ndoa za utotoni haziondoi hali ngumu ya kiuchumi bali hukuza mzunguko wa umaskini, sambamba na kuongeza ufahamu wa sheria zilizopo na utekekelezaji wake ilikuwa ni moja ya mambo yaliyoorodheshwa kama masuala yanayosaidia  kuwalinda wasichana dhidi ya ndoa za utotoni.

“Zanzibar, Save the Children kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti, Jumuia ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA), Kitengo cha Jinsia na Watoto na Mabaraza ya Watoto wamekuwa wakifanya kazi pamoja kuinua ufahamu kuhusu FATWAA dhidi ya ndoa za utotoni kama ilivyotangazwa Agosti 2020 na Baraza la Maulamaa. Save the Children inashiriki kwenye kampeni ya mitandao ya kijamii Zanzibar ikilenga hadhira ya vijana na wazazi ili kuwatia moyo kufanya elimu kuwa kipaumbele na kuchelewa kuingia kwenye ndoa.”

Save the Children inatoa wito kwa wadau wote ikiwamo viongozi wa dini kuungana kufanya kazi pamoja na kuhakikisha masuala anayomlinda msichana dhidi ya ndoa za utotoni yanaimarishwa. Wasichana na wavulana wote wanapaswa kupata elimu bora na kwa kuzingatia makundi ya waliopuuzwa na waliotengwa hususani wasichana.

Elimu inayotolewa inapaswa kuwapatia Watoto maarifa na ujuzi wa maisha kama utambuzi binafsi na uthabiti ili kuwaandaa kuingia kwenye utu uzima. Nyumbani panapaswa kuwa mahala salama kwa Watoto wote. Familia zapaswa kusaidiwa kudumisha makazi tulivu yasiyo na migogoro kwa Watoto wote hususani wanaobarehe na kuvunja ungo ili kuhakikisha wanafurahikukaa nyumbani.

Mfumo wa sheria yapaswa uendane na dhamira ya kimataifa ya Tanzania ya kuzingatia na kutekeleza Tamko la Kimataifa la Haki za Mtoto pamoja na Tamko la Maputo la 2003 kuhusu kutokomeza ndoa za utotoni.

Save the Children itaendelea kuimarisha na kuunga mkono serikali ya Tanzania kufanya kazi kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kufikia dhumuni la ustawi wa watoto sambamba na Tamko la Kimataifa la Haki za Mtoto na Ajenda 2040, ikiwa ni matamanio ya kuifikia Afrika ifaayo kwa watoto.

Save the Children imedhamiria kuendelea kufanya kazi kwa kuonyesha namna, katika muktadha tofauti, na kwa mbinu jumuishi jinsi inavyoweza kwa ufanisi kuondoa vizuizi vya kijamii, kisiasa na kiuchumi ambavyo vimechochea kuwatenga watoto na wasichana wasifikie ukamilifu wao.

Msichana Initiative

Mwaka 2016, Msichana Initiative Organization ilifungua shauri  ahakama Kuu ya Tanzania kuomba kubatilisha vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa, 1971 kwa kuvunja haki ya msingi inayolindwa na katiba na hivyo kumnyima mtoto wa kike fursa kama vile haki ya elimu.

Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja za Msichana Initiative na kuamua kwamba vifungu hivyo ni batili na kinyume na katiba. Hata hivyo, mwaka 2017 serikali kupitia Mwanasheria Mkuu ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Oktoba, 2019 Mahakama ya Rufaa iliridhia uamuzi huo wa Mahakama Kuu na kuiamrisha serikali kupitia bunge ifanye mabadiliko ya sheria husika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Huu ulikuwa uamuzi muhimu sana kuhusu haki za msichana Tanzania na nafasi adhimu kuchochea haki na maendeleo ya msichana pande zote za Tanzania.

Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa unapaswa kuchochea mabadiiliko ya Sheria ya Ndoa, 1971, (Kama ilivyorejewa mwaka 2009) hususani vifungu vya 13 na 17.

Tunatoa wito kwa serikali kuharakisha marekebisho ya Sheria ya Ndoa kwakuwa pasipo kufanya hivyo asilimia thelathini na moja (asilimia 31) ya wasichana wataendelea kuingia kwenye ndoa za utotoni kabla ya umri wa miaka 18 na asilimia tano (asilimia 5) kabla ya umri wa miaka 15.

Kulingana na utafiti wa sasa, uwepo wa ndoa za utotoni ni mkubwa kwenye mikoa ya Shinyanga (asilimia 59), Tabora (asilimia 58), Mara (asilimia 55) na Dodoma (asilimia 51).

Uwepo wa ndoa za utotoni ni mdogo Iringa (asilimia 8) na Dar es Salaam (asilimia 17). Kwa kuhitimisha, Mnaweza wote kufahamu kwamba kuna vichocheo bainifu viwili vya ndoa za utotoni Tanzania.

Kichocheo cha kwanza kinahusiana na kanuni na desturi ambazo zinajumuisha na tabii za Jamii pamoja na kanuni zihusianazo na ndoa, ushirika na uchaguzi biinafsi.

Pili ni kichocheo cha kimuundo kinachojumuisha kipato, umaskini na utegemezi wa kiuchumi; matamanio ya uzazi kwa watoto anaopevuka; upatikanajii wa huduma ya afya ya uzazi na kujamiiana, upatikanaji wa elimu na nafasi za masomo; na mfumo wa sheria. Tofauti za kijiografia pia zinaweza kuleta tofauti za kitamaduni baina ya mikoa na maeneo tofauti.

Taarifa kwa Wahariri

C-Sema ni shirika lisilo la kiserikali linalojikita kuendeleza na kulinda haki za Watoto nchini Tanzania. C-Sema inataka kuona Tanzania ambayo haki za watoto zikiheshimiwa.

Mradi wa kimkakati wa C-Sema ni Huduma ya Simu kwa Mtoto. Huduma ya Simu kwa Mtoto hupokea simu 3,597 kila siku na kutoa msaada wa kitaalamu katika maeneo matatu muhimu ikiwemo Ulinzi na Usalama wa mtoto, Afya na Elimu kwa masaa 24 kila siku.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na: Michael Marwa, Mkurugenzi Huduma ya Simu kwa Mtoto:  [email protected], (+255) 784 842 764.

Kuhusu Save the Children in Tanzania

Shirika limekuwa likifanya kazi zake tangu mwaka 1986.

Save the Children ilianzia Zanzibar ikifanya kazi kwenye eneo la afya ya mama na mtoto. Makao makuu ya shirika yapo Dar es Salaam, Save the children inafanya katika mikoa 10 nchini (Dar es Salaam, Zanzibar –Unguja na Pemba, Shinyanga, Morogoro, Dodoma, Kigoma, Rukwa, Iringa, Songwe na ikiwemo katika kambi za wakimbizi Nyarugusu na Nduta

Tanzania kazi yetu imejikita katika maeneo yafuatayo:

  •  Afya na Lishe
  •  ELimu Ulinzi wa Mtoto
  •  Usimamizi wa Haki za Watoto
  •  Riziki

Kwa taarifa zaidi wasiliana na: Wilbert Muchunguzi,

Mtaalam wa Haki za Watoto na

+255765254572

Kuhusu Msichana Initiative

Msichana Initiative ni Shirika lisilo la kiserikali linalo tetea haki ya Elimu kwa mtoto wa kike. Juhudi zinalenga kuhakikisha haki ya elimu inatolewa kwa usawa bila ubaguzi kupitia kuboresh Maisha ya mtoto wa kike kwa kuongeza upatikanaji wa fursa za elimu, kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa mtoto, kuwezesha uppatikanaji wa huduma za hedhi salama Pamoja na kuendeleza harakati za mabadiliko ya sheria na sera zinazolenga maslahi yam toto wa kike.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na: Rebeca Gyumi, Mkurugenzi

Msichana Initiative: [email protected],

(+255) 762 758 281

Kuhusu #SikuYaMtoto: Mwaka1991, wakuu wa nchi wanachama wa OAU walianzisha #SikuYaMtoto wa Afrika (DAC) kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wanafunzi 16 Juni 1976 huko Soweto, Afrika Kusini. Wakati huo, wanafunzi  waliandamana dhidi ya elimu duni ya kibaguzi waliyopea na serikali ya kibeberu na kuomba kufundishwa kwa lugha zao wenyewe.

Msichana Initiative, Save the Children, JengaHub, Women Fund Tanzania na C-Sema wanaungana na ulimwengu katika  kuadhimisha siku hii inayolenga kuendeleza haki za mtoto, kuainisha mapungufu yaliyopo kwenye usawa wa kijinsia yaliyopo kati yam toto wa kike na wa kiume na kuonesha aina mbali mabali za ubaguzi na ukatili wanaoupitia Watoto wa kike na wa kiume duniani kote.

Ndoa za utotoni ni suala la linalo mnyima mtoto wa kike kufurahia haki zake kikamilifu na kutunza utu wake.

Muhimu zaidi, tunayo furaha kuwaleta pamoja Watoto watakaokutana leo baadae kupitia zoom kujadili mada isemayo, Tanzania salama bila ndoa za utotoni: Nini kifanyike?

Tukio litahudhuriwa na Watoto wenye umri kati ya miaka 11 na 15 kuanzia saa 4 asubuhi, kutakuwa na uwakilishi wa Watoto kutoka maeneo mabalimabali ya nchi ikiwemo Zanzibar, Kanda ya Pwani. Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Kaskazini, kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati.