Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bonite Bottlers yang’ara Tuzo za 18 za Rais za Mzalishaji Bora Viwandani

Novemba 8, 2024 katika Ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Bonite Bottlers iliweka his­toria nyingine baada ya kushinda tuzo ya Rais ya mzalishaji bora viwandani.

Kampuni hiyo imefanikiwa kupata tuzo za Rais za Mzalishaji Bora Viwanda ikishinda katika kipengele cha mzalishaji bora wa vinywaji visivyo na kilevi nchini.

Tuzo hizi, ambazo hutolewa na Shirik­isho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa kushirikiana na wadau wengine zinalenga kuenzi juhudi za wazalishaji wa ndani wanaochangia uchumi wa Taifa kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na zenye thamani kwa watumiaji wa ndani na nje ya nchi.

Bonite Bottlers, ambayo ni maarufu kwa uzalishaji wa vinywaji kama maji ya kuny­wa ya Kilimanjaro, soda za Coca-Cola na jamii yake, na vinywaji vingine visivyo na kilevi, imekuwa ikitambuliwa kwa kujitu­ma katika kuhakikisha kuwa bidhaa zake zinakidhi viwango vya kimataifa.

Bidhaa zao zimekuwa na sifa ya ubora, usalama na ladha inayovutia watumiaji wa rika zote. Maji safi na salama ya kuny­wa, kama vile Kilimanjaro Drinking Water ni baadhi ya bidhaa zinazopendwa zaidi, si tu Tanzania bali pia katika nchi za jirani.

Mafanikio ya Bonite Bottlers katika tuzo za 18 za Rais za Mzalishaji Bora Viwandani yanathibitisha mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa Tan­zania, kuboresha maisha ya watumiaji na kuhamasisha viwanda vingine kuwekeza katika ubora wa bidhaa na teknolojia bora.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, gazeti hili lili­fanya mahojiano na Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Bonite Bottlers, Chris­topher Loiruk ambapo alieleza kwa undani mambo yaliyosababi­sha kuibuka mshin­di wa tuzo hiyo. Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo;


Bonite Bottlers imekuwa moja ya chapa za kua­minika, Tanzania, Afrika Mashari­ki na Afrika kwa ujumla. Nini siri ya mafanikio haya?

T u m e k u w a tukizalisha bidhaa bora kwa kuzin­gatia viwango vya kitaifa na kimataifa lakini pia uwekeza­ji katika mitambo inayotumia tekno­lojia kisasa.

Tumeweke­za katika mitambo ya kisasa inayo­hakikisha ufanisi mkubwa na kulinda mazingira, jambo ambalo linatambulika kama sehemu ya utunzaji wa mazingira na afya ya jamii.

Kwa kutumia teknolojia za kisasa na mfumo wa uzalishaji unaozingatia uhi­fadhi wa maliasili, tumeweza kuonge­za kasi ya uzalishaji, jambo ambalo limewezesha upatikanaji wa bidhaa bora kwa bei nafuu.


Bonite Bottlers inajitofautisha vipi sokoni kupitia chapa zake mbalimbali inazozal­isha?

Kwa kutoa huduma bora kwa wateja wetu, kwa kuwapa wateja wigo mpana wa bidhaa kuendana na mahitaji yao lakini pia kwa kuweka ukaribu na wateja kupitia wawakilishi wetu wenye weledi sehemu mbalimbali.

Hongereni kwa kutunikiwa tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora Viwandani. Tuzo hii ina maana gani kwenu?

Tuzo hii ina maana kwamba wateja wetu na jamii nzima ya Watanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla wana imani kubwa na bidhaa zetu.

Pia tuzo hii ni ushahidi wa jitihada kub­wa za kampuni kuhakikisha kwamba kila bidhaa tunayozalisha inatimiza viwango vya ubora unaotakiwa. Lengo letu kuu ni kutoa bidhaa bora kwa watumiaji huku tukizingatia afya ya jamii na utunzaji wa mazingira.


Hii ni mara ya ngapi Bonite Bottlers kupa­ta tuzo hii na nini siri ya mafanikio haya?

Ni mara ya tatu kupata tuzo hii na siri ya mafanikio yetu ni kuzalisha bidhaa bora kutoka chanzo cha maji asili na cha kipe­kee hivyo kupelekea wateja wetu kutua­mini na kutuchagua.

Nini kinafuata baada ya Bonite Bottlers kushinda tuzo hii?

Ni kuhakikisha tunaendelea kuzalisha bidhaa bora na kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wetu na pia kubaki katika ubo­ra ule ule wa kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Kwa kiasi gani tuzo hii itaongeza hamasa katika kuendelea kutoa bidhaa bora zin­azokidhi mahitaji ya wateja wenu?

Tunategemea kuendelea kuzalisha bidhaa bora kwa kutumia mitambo inayo­tumia teknolojia ya kisasa hivyo kuen­delea kuboresha wigo wa bidhaa zetu ili kuwafikia zaidi wateja wengi wa kada mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji yao yanayo badilika mara kwa mara kuendana na wakati.


Bonite Bottlers mnakabiliana vipi na changamoto ya kughushi bidhaa ambayo imekuwa ikiwakabili wazalishaji wengi wa ndani?

Tuna mtandao mkubwa wa wauza­ji wetu na mawakala nchi nzima hivyo inatupa nafasi kuweza kubaini kwa haraka kama kuna changamoto yoyote kwenye bidhaa zetu na kuifanyia kazi.


Nini kifanyike ili kuhakiki­sha changamoto hii ina­pungua kama sio kuisha kabisa?

Kwanza ni kuhakikisha uzalishaji wa bidhaa hautoi mwanya wa watu kuweza kughushi kwa kuweka ala­ma mbalimbali za usalama wa bidhaa.

Pili ni kuwa na ufuatiliaji wa karibu kupitia wafanya­k a zi wa k a m ­p u n i kwenye sehemu za biasha­ra kufanya uhakiki wa mara kwa mara wa bidhaa zinazo uzwa.

Na mwisho ni kwa jamii yetu kufichua wale wote wanaojihusisha na pia kughushi taarifa zisizo kweli kuhusu makam­puni pamoja na bidhaa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria


Mbali na kushinda tuzo hii, ni mafanikio gani mengine mnajivunia mpaka sasa?

Bonite Bottlers ni moja ya kampuni iliyo karibu na jamii ya Kitanzania katika kufadhili matukio mbalim­bali ya kijamii kama vile michezo na burudani. Ime­kuwa pia ikishiriki kusaidia jamii pale inapopatwa na changamoto mbalimbali.

Tuzo za 18 za Rais za Mzalishaji Bora Viwandani zilitoloewa katika hafla ili­yofanyika Novemba8, 2024 kwenye Ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muun­gano wa Tanzania, Dk Phil­ip Mpango.