Carbon Tanzania yakabidhi Sh 4.7 bilioni kwa serikali za mitaa, jamii

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (katikati) akiwa katika picha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga (wa nne kulia) Mkurugenzi wa fedha wa Carbon Tanzania, Alphael Jackson (wa nne kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Kheri James (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Manyara mara baada ya kupokea hundi ya Sh 4.7 bilioni kutoka kampuni ya Carbon Tanzania.
Fedha hizo ni mapato yanayotoka kwenye maeneo ya miradi ya Yaeda-Eyasi na Makame Savannah mkoani Manyara.
Ili kuleta manufaa kwa wananchi wake na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi Serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ushirikiano huo umekuwa ukisaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata fursa za kujitengenezea vipato kuto¬kana na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hizo.
Kampuni ya Carbon Tanzania ni miongoni mwa taa¬sisi zinazoshirikiana kwa karibu na Serikali kupitia utekelezaji wa miradi yake.
Carbon Tanzania ni kampuni ya kitanzania ambayo imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kukuza uchumi wa nchi na watu wake kwa kutoa thamani katika rasilimali asilia kwa jamii za vijijini kupitia usimamizi endelevu wa misitu na uto¬fauti wa viumbe hai.
Kampuni hiyo imekuwa ikizalisha thamani katika uchumi wa Tanzania pamo¬ja na wananchi wake kwa kuwapatia fidia ya kaboni inayotokana na misitu asili, ambayo inawawezesha watu wa jamii hizo kupata mapato kutokana na ulinzi wa misitu yao.
Upunguzaji huu wa hewa ya kaboni huruhusu soko la kimataifa lenye kupunguza uzalishaji wa kaboni kutumia mikakati bora ya nishati ya kaboni inayoaminika na hali chanya ya asili kuwekeza katika suluhisho la asili lin¬alozalishwa nchini ambalo linahudumia jamii, hali ya hewa na wanyamapori.
Carbon Tanzania hushirikiana na jamii zinazozun¬guka misitu na kuhakikisha jamii hizo zinakuwa wasimamizi wazuri wa misitu kupitia mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyotenegenzwa na jamii zenyewe.
Carbon Tanzania hufanya kazi kama kiungo muhimu kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa ili kuwezesha jamii ya kitanzania kupata mapato kutokana na ulinzi wa misitu na wanyamapori.
Kupitia utekelezaji wa miradi yake ya Yaeda-Eyasi na Makame Savannah, Novemba 14, 2023 Carbon Tanzania ilikabidhi hundi ya Sh4.7 bilioni ikiwa ni fedha zitokanazo na utekelezaji wa miradi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja.
Hundi hiyo ilikabidhiwa na Mkurugenzi wa fedha wa Carbon Tanzania, Alphael Jackson kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ambaye aliikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga kwa niaba ya uongozi na wananchi wa halmashauri za wilaya za Mbulu na Kiteto wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya White Rose, wilayani Babati mkoani Manyara.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Manyara wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa jamii ya Wadatooga kutoka Bonde la Yaeda Eyasi.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo; Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Kheri James, viongozi wengine wa Serikali na wananchi.
Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Carbon Tanzania, Marc Baker anasema kampuni hiyo imekuwa ikifanya biashara na jamii zinazozunguka misitu.
“Shughuli zetu kubwa tunazifanya kwa kushiriki¬ana na jamii na Serikali hivyo kupitia fedha tunazozalisha kutokana na utekelez¬aji wa miradi yetu tumekuwa tukitenga sehemu ya mapato ghafi kila mwaka kwa ajili ya kuzipeleka kusaidia kati¬ka utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii,” anas¬ema Baker.
Anasema kiasi cha fedha Sh 4.7 bilioni walichokabi¬dhi ni fedha zilizotokana na utekelezaji wa miradi ya Yae¬da Eyasi na Makame Savan¬nah ya mkoani Manyara kwa mwaka 2022/2023.
“Kwa biashara hii Serikali za vijiji kupitia wananchi wao wameweza kubore¬sha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya, elimu, maji na miundombinu jambo ambalo ndilo lengo letu kub¬wa la kunagusa maisha ya wana jamii,” anasema Baker.
Anasema kwa kiwango cha juu, biashara ya vyeti vya fidia ya uzalishaji wa kaboni inahusisha jamii zinazozun¬guka misitu katika mfumo wa fedha wa kimataifa na upatikanaji wa pesa katika mfumo huo.
“Miradi yetu inatambua jukumu muhimu la jamii za wazawa na inategemea ush¬iriki wao kikamilifu. Kupitia kufanya maamuzi shirikishi, jamii husika huamua mgao wa mapato hayo kufanikisha mipango ya kijamii kama vile kujenga shule au vituo vya afya,” anasema Baker.
Mradi wa Bonde la Yaeda- Eyasi
Mradi huu ulianzishwa mwaka 2012 huku mapato ya kwanza ya kaboni yakipati¬kana mwaka 2013. Lengo la mradi huu ni kuhifadhi msitu ambao ni makazi ya asili ya Hadza ambao ni wawindaji na Datooga ambao ni wafugaji kwa kuanzisha umiliki wa maliasili katika makazi yao na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya uvamizi.
Mwaka 2021, Mradi wa Yaeda-Eyasi uliongezeka kwa kujumuisha vijiji 12 kwa jumla. Kwa sababu hii na kuongezeka kwa mapato ya kaboni, jamii za Mradi wa Yaeda-Eyasi ziliweza kuajiri wafanyakazi zaidi ili kuhakikisha wanaweza kulinda misitu yao iliyokuwa kwenye hatari.
Mwaka 2021, askari 115 wa uhifadhi ngazi ya kiji¬ji waliongezwa ikiwa ni pamoja na wahasibu wawili na Mratibu mradi mmoja waliajiriwa katika vijiji vyote tisa. Nafasi hizi mpya ziliun¬dwa ili kuhakikisha msitu wa jamii unalindwa ipasavyo na kila mwanajamii ananufaika kutokana na fidia.
Mradi Makame Savannah
Mradi huu ulianzishwa mwaka 2016 huku mapato ya kwanza ya kaboni yakipati¬kana mwaka 2020. Malengo ya mradi huu ni kuhifadhi makazi muhimu ya wanya¬ma kwa kushirikisha jamii ya Wamasai kuunda mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi utakao boresha afya ya mifu¬go, wao wenyewe pamoja na mfumo mzima wa ikolojia.
Jumuiya ya Mradi wa Makame zililenga katika kuboresha nyenzo za elimu katika kipindi chote cha mwaka 2022. Bweni la wasi¬chana lilijengwa ili kunusuru watoto wa kike wapatao 70 ambao wangeshindwa kue¬ndelea na masomo kutokana na mila na desturi zinazop¬inga wasichana wasishiriki elimu ya bweni pamoja na wavulana.
Vilevile, Jumuiya hiyo imetumia fungu la fidia yao ya kaboni, kulipa ada kwa wanafunzi zaidi ya 100 wanaosoma vyuo mbalim¬bali nchini ili kuhimiza elimu jumuishi kwa ngazi zote.
Miradi ya Carbon Tanza¬nia inalenga kuhifadhi misitu katika maeneo ambayo jamii husika hazikuwa na uwezo wa kutambua thamani ya misitu yao ya asili.