Carbon Tanzania yatoa ripoti ya utekelezaji na mafanikio katika miradi yake na jamii kwa mwaka 2023

Daktari akitoa huduma kwa mgonjwa katika hospitali ya Kapanga.

• Mapato ya kiasi cha Sh 18.3 bilioni kwa vijiji na jamii zinazozunguka maeneo ya misitu ya miradi kupitia ushiriki wa soko la hewa ukaa - ongezeko la zaidi ya asilimia 50 kulinganisha na mapato ya mwaka 2022

• Jumla ya eneo la hekta 690,500 za misitu iliyolindwa.

• Tani 899,825 za kaboni (CO2) zimeokolewa kutoka katika miradi ya ulinzi wa misitu ya Carbon Tanzania - sawa na kuondoa uchafuzi wa kaboni izalishwayo na magari zaidi ya laki 2 kwa mwaka mmoja.

• Kwa kutumia zana mpya ya upimaji wa thamani ya kijamii katika mradi wa bonde la Yaeda, ilibainika ya kuwa wanajamii wanapata ongezeko kubwa la thamani ya maendeleo yao kwa kiwango kikubwa kuliko thamani ya kiwango cha uwekezaji kilichowekwa na Carbon Tanzania.

Carbon Tanzania, ambayo ni kampuni kinara katika ulinzi wa misitu Tanzania na mapato ya hewa ukaa, imetoa ripoti yake mpya ya mafanikio kwa mwaka 2023, inayoonyesha maendeleo makubwa katika maeneo ya kijamii na kimazingira.

Katika mwaka ulioshuhudia ukuaji na mafanikio makubwa, vijiji pamoja na jamii wakishirikiana na Carbon Tanzania, wamejipatia zaidi ya kiasi cha Sh 18.3 bilioni katika mapato kwa vijiji na jamii zinazozunguka misitu kwenye maeneo ya miradi yao, kupitia soko huria la hewa ukaa(Voluntary Carbon Market – VCM).

Mapato haya yanawezesha jamii za pembezoni mwa misitu kusimamia rasilimali zao za misitu kwa njia endelevu na kuwekeza katika afya, elimu na miundombinu muhimu. Hii huongeza usalama kwa maeneo ya hifadhi kwa baadhi ya wanayamapori maarufu zaidi barani Afrika.

Kwa upande wa bionuwai ya Tanzania, pia imeonyesha mabadiliko chanya na makubwa, kwani miradi ya Carbon Tanzania huko Yaeda – Eyasi, Makame na Ntakata, imeweza kulinda misitu yenye makazi ya wanyamapori, yenye ukubwa sawa na hekta 690,500.

Juhudi hizi za uhifadhi zilisababisha kuokolewa kwa tani 899,825 za hewa chafu ya kaboni, sawa na kuondoa uchafuzi wa kaboni izalishwayo na magari zaidi ya laki 2 kwa mwaka mmoja.

Mafanikio ya kijamii katika juhudi za uhifadhi wa misitu

Watoto wa jamii ya Makame Maasai.

Ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kupima thamani ya kijamii, Carbon Tanzania ilifanya tathmini ya kina ya mafanikio na maendeleo ya kijamii katika Bonde la Yaeda, kwa dhumuni la kupata ufahamu haswa wa thamani ya kijamii kupitia mapato ya mradi huu wa hewa ukaa.

Kwa kutumia mbinu madhubuti ya Mrejesho wa Kijamii kwenye Uwekezaji (Social Return on Investment - SROI), tathmini ilichunguza kwa kina njia ambazo mapato ya hewa ukaa yalitafsiriwa kulingana na maendeleo mbalimbali ya kijamii yanayoweza kuonekana dhahiri.

Manufaa hayo kama vile; kilimo, na hali ya ufugaji iliyoimarishwa, vinahamasisha uendelezaji wa ulinzi wa misitu. Zana hii mpya ya kupima thamani ya kijamii, itatumika pia kupima maendeleo ya kijamii kwa miradi mingine ya Carbon Tanzania katika mwaka wa 2024.

Akizungumzia ripoti hiyo, Marc Baker, Mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Carbon Tanzania alisisitiza mbinu jumuishi ya shirika hilo kuhusu uhifadhi akisema: “Kazi yetu ni zaidi ya kulinda misitu, inahusisha pia kuwezesha jamii, kuhifadhi bioanuwai na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tunaamini kwamba kupitia kusikiliza na kuimarisha sauti za wanajamii wazawa pamoja na kupima faida za kijamii, tunaweza kuweka msingi wa mfumo wa kiuchumi unaothamini mazingira.”

Taarifa fupi ya miradi ya Carbon Tanzania kwa mwaka 2023: Kuwawezesha wanawake na kuimarisha uhifadhi

Miradi ya Carbon Tanzania kwa mwaka 2023 ilihusisha kutoa mafunzo na kuajiri wanawake watano katika mradi wa Makame Savannah kama walinzi wa misitu wa vijiji (Village Game Scouts - VGS), hii ilisaidia sio tu kuondoa dhana potofu za kijinsia, bali pia ilihimiza juhudi shirikishi za uhifadhi.

Kamati ya Maliasili ya Kijiji cha Lugonesi.

Katika mradi wa Milima ya Ntakata, mapato yanayotokana na mradi wa hewa ukaa yaliwezesha mikopo kwa wanawake 189 na kuwawezesha kuanzisha biashara zinazozingatia uhifadhi. Mpango huu uliangazia moja kwa moja vikwazo vya kihistoria vya upatikanaji wa fedha kwa wanawake kwenye jamii.

Na katika mradi wa Uwanda wa Ruvuma, wasimamizi wa mradi walipata mafunzo ya mpango na mfumo wa kisasa – Cluey, uliyoundwa kulingana na shughuli za mradi zinazoongozwa na jamii ili kuongeza maarifa na ufanisi wa mradi.


Kuhusu Carbon Tanzania

Carbon Tanzania ni kampuni ya kitanzania inayoongeza thamani katika rasilimali asilia kwa jamii za vijijini kupitia usimamizi endelevu wa misitu na kwa kulinda bionuwai.

Tunaongeza thamani katika uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla kwa kutoa fidia kwa misitu ya asili inayowawezesha wanajamii husika kujitengenezea kipato kutokana na uhifadhi wa maeneo yao.

Upunguzaji huu wa hewa ukaa ulio idhinishwa huruhusu makampuni ya kimataifa yenye dhamana ya kupunguza uzalishaji wa kaboni dioksaidi, kwa kuzingatia mbinu Rafiki za Kiasili na zinazoaminika, kuwekeza katika miradi ya kijamii inayolenga kuleta suluhisho la asili linaloleta manufaa kwa hali ya hewa, jamii na wanyamapori.


Kwanini Carbon Tanzania

Uaminifu

Carbon Tanzania ni mshirika wa kuaminika na kutegemewa katika kuunga mkono jitihada za kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazoongoza duniani katika uhifadhi wa misitu, pamoja na kuleta fursa ya fedha za kigeni zitakazo wanufaisha wananchi kwa kiwango kikubwa.

Wanawake wa kijiji cha Endesh katika eneo la Yaeda Eyasi wakiandaa chakula.

Ongezeko la thamani

Tunatoa fidia za kifedha za mara kwa mara na za kuaminika kwa wanakijiji na wanajamii wa eneo husika, hali inayochochea ukuaji wa uchumi vijijini na kupelekea kuongezeka kwa pato la taifa

Ulinzi wa rasilimali

Tunaunganisha jamii na mifumo ya kifedha ya kimataifa kwa kupitia uthibitishaji wa fidia ya kaboni inayowezesha jumuiya za uhifadhi (WMA) kujipatia kipato kutokana na uhifadhi wa misitu ya asili. Hivyo badala ya kuathiriwa na uhifadhi, jamii inanufaika kwa kujitolea kusimamia na kuhifadhi rasilimali.


Jamii za wazawa

Wazawa wa eneo husika ndio wasimamizi wazuri zaidi wa maliasili. Wakipatiwa haki za uhakika dhidi ya rasilimali zao za asili na kufidiwa ipasavyo kutokana na juhudi zao za uhifadhi, hivyo basi matokeo mazuri Zaidi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanawezekana.


Faida zenye uhalisia

Uhifadhi wa misitu ni mojawapo ya njia rahisi yenye gharama nafuu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na huleta manufaa chanya yanayoweza kupimika kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa jamii husika. Fidia ya kaboni huzuia ukataji miti hovyo, hulinda wanyamapori na kunufaisha jamii.