CRDB: Hii ndiyo nguvu ya ‘buku’ katika vyombo vya moto na afya

Wamiliki wa vyombo vya moto hususan bajaj na bodaboda wame-kuwa wakiishi kwa mashaka muda wote kutokana na ajali za mara kwa mara dhidi ya mali zao wakati huo huo wanashindwa kumudu gharama kubwa za upatikanaji wa huduma za bima kwa ajili ya vyombo hivyo, mpaka pale mkombozi wao, Benki ya CRDB ikishirikiana na kampuni za bima, ilipokuja na bidhaa mahsu-si kwao ijulikanayo ‘Bima ya Buku.’

‘Bima ya Buku’ ndiyo bidhaa nafuu ya bima kuwahi kutokea nchini inay-omwezesha mmiliki wa bodaboda au bajaji kukilinda chombo chake dhidi ya ajali ama kuibiwa pamoja na afya.

Tofauti na utaratibu uliozoeleka wa ulipaji wa michango ya bima kwa mkupuo mmoja, bima hii mchangia-ji analipa kuanzia Sh 1,000 kila siku mpaka atakapokamilisha gharama za bima hiyo na wakati huo huo akiendelea kunufaika na bima hiyo, anasema, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.

Bima ya Buku inapatikana kati-ka madaraja manne nayo ni; bima ndogo, bima ndogo na afya, bima kubwa, na bima kubwa na afya.

Faida zipatikanazo na bima hii ni ulinzi dhidi ya vyombo vya moto yaani bodaboda na bajaji, ulinzi kwa ajili ya abiria na watumiaji wa barabara. “Kwa kutumia na bima hii, mteja anajihakikishia matibabu katika hospitali yoyote ya Serikali nchini endapo atapata janga, mfano kuugua ghafla au kupata ajali.

”Raballa anasema, “Bima hii itaku-wezesha kupata fidia pindi unapo-tokea uharibifu wa chombo chako cha moto.”Baada ya kukata bima, mmiliki ataanza kunufaika na bima ya afya itakayoanza kutumika siku 30 baada ya kujiunga na bima hiyo, anaeleza Raballa.

Pia ni fursa ya kupangilia kipato na mkataji bima ataunganishwa na bima ya maisha itakayolipa mkopo endapo mmiliki wa bima atafariki.


Raballa anasema kuwa bima hiyo inapatikana mahali popote na wakati wowote. “Hivi sasa wateja wanaweza kukata bima kupitia simu zao za mkononi kwa njia ya SimBank-ing kwa kupiga namba *150*03# na kuchagua namba 3. Baada ya malipo tu, utatumiwa ujumbe mfupi wa uthibitisho na kupata tiketi ya dha-habu papo hapo.”

“Uzuri wa marejesho yake hufanyika kwa siku. Marejesho yanaweza kulipwa kwa siku nyingi zaidi kadri kipato cha mmiliki kina-vyoongezeka,” anaeleza zaidi.Raballa anasema wazo la kuja na bidhaa hiyo limetokana na uhitaji wake mkubwa kwa jamii kwa sasa na changamoto ya gharama za bima katika jamii.

Alipoulizwa kuhusu mwitikio wa bima hiyo, anasema: “Mwitikio umekuwa mkubwa sana kwa sasa hasa baada ya ongezeko la wigo wa elimu ya bima inayotolewa kupitia mabenki ambayo yanajishughulisha na uwakala wa bima.

Bidhaa hii inaifanya Benki ya CRDB kukuza soko la bima nchini ambapo kulingana na utafiti wa FSDT, ni asilimia 10 tu ya Watanza-nia ambao wamefikiwa na huduma za bima.