GGML inavyochochea mabadiliko chanya ya kimazingira ili kuhakikisha dunia endelevu
Juni 5 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya Mazingira. Lengo la siku hii ni kutunza na kuboresha mazingira pamoja na kuangazia changamoto kuu za mazingira ambazo dunia inakumbana nazo.
Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ambayo ni kampuni tanzu ya AnglogoldAshanti ni moja ya kam-puni iliyoko nchini na imekuwa ikichochea mabadiliko chanya ya kimazingira ili kuhakikisha dunia endelevu.
Moja ya tunu za kampuni ya GGML ni kuhakikisha uende¬levu unakuwepo hasa katika mazingira, jamii inayowazunguka pamoja na uendelevu wa masuala ya kiuchumi.
Hii sio kwa wafanyakazi wa GGML pekee bali wanahakikisha hata wale wanaofanya kazi kwa niaba yao, wanapaswa kulinda mazingira kama moja ya tunu za kampuni.
GGML ina sera ya mazingira ambayo ina mambo mbalimbali lakini kubwa likiwa kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kutii sheria zote zinazohusu mazingira zilizopo nchini.
Zipi juhudi za GGML katika kulinda mazingira?
Kwa mujibu wa Meneja wa Mazingira wa GGML, Yusuph Mhando ili kuhakikisha mazingira yanakuwa salama upo utamaduni wa kutoa elimu ya mazingira kwa wafanyakazi na wadau wengine ikiwemo jamii inayozunguka mgodi.
Kwa kushirikiana na mam¬laka za Serikali ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji na Wakala wa Misitu nchini (TFS), GGML hufanya kazi kwa karibu kuhakikisha mazingira yanakuwa salama na endelevu.
Mhando anasema kampuni hiyo ina vibali vyote vya maz¬ingira vinavyohitajika lakini katika kuhakikisha mazin¬gira yako salama wamekuwa wakipima kubaini vihatarishi vya kimazingira mapema kabla ya kazi kufanyika ili kudhibiti uharibifu wa mazingira endapo utakuwepo.
Kama ilivyo ada, shughuli za mgodi hutegemea ardhi ambayo nayo ina vyanzo vya maji hivyo wao kama GGML huhakikisha wanalinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuhakikisha shughuli zinazofanyika haziathiri kwa vyovyote vyanzo vilivyopo chini au juu ya ardhi.
Kipi kinafanyika kuhakikisha mazingira yanakuwa salama hata baada ya kumaliza shughuli za uchimbaji?
Ipo mipango mbalimbali ya usimamizi wa mazingira inayosimamiwa na GGML katika kuhakikisha mazingira yanaku¬wa salama na endelevu hata baada ya shughuli za uchimbaji kumalizika.
Moja ya mipango hiyo ni ule wa usimamizi wa ubora wa maji, kutokana na maji kutiririka endapo hayatasimamiwa vizuri yanaweza kuchafuka wakati wa shughuli za mgodi na kwenda kwenye mazingira na jamii inayotumia maji hayo hivyo kusababisha madhara.
Kupitia mpango huo, GGML wanahakikisha wanalinda na kuzuia uchafuzi wa maji unaotokana na shughuli za mgodi.
Amesema wamekuwa waki¬fanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuona namna ya kuboresha na kulinda uchafuzi wa maji kwani kupitia kupima ubora wa maji husaidia kut¬ambua kama kuna uchafuzi na kuufanyia kazi ili usiendelee kuwepo.
Mbali na mpango wa usi¬mamizi bora wa maji, upo mpango wa usimamizi wa hewa ambao lengo lake ni kusimamia hewa ukaa inayoza-lishwa kwenye mashine zinazo¬tumika ndani ya mgodi ambazo zinaweza kuchafua mazingira.
Kupitia mpango huo, endapo kutatokea hewa inayochafua mazingira, hewa hiyo hudhibiti¬wa mapema na kuhakikisha hewa ukaa inayozalishwa iko ndani ya matakwa ya kisheria.
“Tumekuwa pia tukifanya ukaguzi maeneo ya kazi ili kama kuna mahali penye ucha¬fuzi hata kama ni kidogo kuona namna ya kuboresha na kulin¬da huo uchafuzi usiendelee. Tunapima ubora wa hiyo hewa na kujihakikishia vifaa vya kud¬hibiti vinafanya kazi vizuri,” amesema Mhando.
Upo pia mpango wa upimaji kelele na mitetemo, kwani shughuli za uchimbaji madini hutegemea ulipuaji wa miamba ambapo unapofanyika hutokea kelele na mitetemo na ili kuhakikisha inakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa, mit¬ambo maalum hupima ili kut¬ambua na kurekebisha vigezo vya ulipuaji ili viwe ndani ya vile vinavyotakiwa kisheria.
Mpango wa usimamizi wa kemikali, GGML wamekuwa wakihakikisha kemikali zote zinazotumika mgodini zinasa¬firishwa kuhifadhiwa na kutu-miwa kwa kuzingatia usalama kwa mujibu wa sheria wakati wote.
Ili kuhakikisha kemikali haz¬ichafui mazingira kumekuwa na utamaduni wa kufanya ukaguzi kwenye maeneo ya uhifadhi na kuangalia namna ya uta¬ratibu unavyofuatwa pamoja na kuhakikisha vibali vyote vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria vinakuwepo.
Usimamizi wa bayoanuai ni miongoni mwa mipango inayo¬tekelezwa na GGML ambao unahusisha kulinda na kuhifadhi msitu uliopo eneo la mgodi na kazi hiyo hufanyika kwa kushirikiana na TFS pamoja na jamii jirani inayowazunguka.
Pia wamekuwa wakitoa elimu ya kuotesha vitalu vya miti na baada ya miche kukua GGML hununua miche kutoka kwenye vitalu vilivyopo kwa jamii na hii pia huisaidia jamii kuingiza kipato kutokana na uuzaji wa miche hiyo.
Tofauti na maeneo mengine ukiwa GGML, huruhusiwi kuwinda, kulisha au kuwapiga wanyamapori walioko ndani ya eneo la mgodi au msitu na itaka¬pobainika mfanyakazi kwenda kinyume na sheria hii, hatua huchukuliwa na mfanyakazi huyo huwajibishwa.
GGML, mbali na kulinda msitu uliopo ili uwe endelevu pia upo mpango wa ukarabati wa ardhi. Mpango huu hutu¬mika kupanda miti kwenye eneo lililoko wazi baada ya kazi kum¬alizika ambapo kwa kipindi cha mwaka 2022-2024 miti zaidi ya 473,000 imepandwa mgodini na kwa jamii zinazozunguka mgodi.
Mbali na kupanda kwenye eneo lililoko wazi mgodini, wamekuwa na utamaduni wa kugawa miche kwa wafanyakazi pamoja na taasisi za umma ambapo kwa kipindi hicho miche takribani zaidi ya 42,000 imetolewa.
“Tumekuwa tukitoa miche ya miti kwa wafanyakazi wetu, jamii inayotunzunguka pamoja na taasisi za umma lengo likiwa ni kuhakikisha sio mazingira ya mgodi pekee yanatunzwa bali mazingira yote ya Geita yanakuwa endelevu na rafiki,” amesema Mhando.
Katika hatua nyingine za kutunza mazingira Kampuni ya GGML imekuwa na mpan¬go wa kupunguza hewa ukaa inayotokana na matumizi ya mashine zinazotumika mgodini kwa kutumia umeme wa mafuta huku wakiwa kwenye hatua za mwisho za mchakato wa kuhama kutoka kwenye umeme wa kutumia mafuta na kuhamia kwenye ule unaozalishwa na TANESCO.
“Ndani ya mgodi tunatumia kemikali za aina mbalimbali na tunahakikisha tunasimam¬ia kemikali hizi kitaalam na kisheria zisiharibu mazingira na inapotokea kuna ajali ya kimazingira lazima ufanyike uchunguzi kutambua sababu na kuweka mikakati ya kurekebi¬sha na kuhakikisha haitokei tena hapo baadae,” amesema Mhando.
Upo pia mpango wa ufungaji mgodi ambao mamlaka za Serikali hushirikishwa pamoja na jamii inayowazunguka lengo likiwa ni hata pale shughuli za uchimbaji zinapomalizika mazingira yaendelee kuwa salama na endelevu.
Naye Meneja Mwandamizi wa masuala ya Afya, Usalama na Mazingiria wa GGML, Dk Kiva Mvungi anasema mbali na mipango yote hiyo, kabla ya kupata kibali cha kuchimba, kampuni yoyote ya uchimbaji hupaswa kuithibitishia Serikali mipango yake ya kuhakikisha itasimamia na kutunza mazingira na itapojiridhisha ndiyo kibali hutolewa.
Kampuni ya GGML kama kampuni nyingine wamekuwa wakitekeleza mpango huo kwa umakini mkubwa kuhakikisha mazingira yanakuwa salama na endelevu.
Akizungumzia uwajibikaji kwa jamii kama ilivyo ada kwa kampuni ya GGML, Dk Kiva amesema kila mwaka kwa kushirikiana na wadau wengine wanapotengeneza mpango wa CSR hutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya masuala ya mazingira.
Ipo miradi ya mazingira ili¬yotekelezwa ikiwemo ununuzi wa mitambo ya kuzolea taka pamoja na matanki maalum za kutunzia taka zilizowekwa kwenye mitaa mbalimbali ya mji wa Geita ili kuwezesha wananchi wa maeneo hayo kutunza uchafu na baada ya muda taka hizo huondolewa.
Amesema kupitia mipango ya uwajibikaji, GGML pia imetoa vifaa vya kuhifadhia taka vilivyowekwa kandokando ya barabara za katikati ya mji ili kuwezesha wananchi kutupa taka badala ya kuzitupa kiholela na kuufanya mji kuwa mchafu.