JICA inasherehekea kukamilika kwa Mpango wa NINJA awamu ya pili (NINJA2) nchini Tanzania

New Content Item (1)

 Capacity Building session

Kusaidia uanzishaji wa biashara za kibunifu zenye manufaa Tanzania

Next INnovation with JApan(NINJA)ni mpango wa kusaidiabiashara zinazokua uliobuniwa kuwezesha wajasiriamali na wafanyabiashara chipukizi katika nchi zinazoendelea ambao wanaanzisha mawazo ya biashara bunifu ili kutatua changamoto za kijamii. Mpango huu wa NINJA unajumuisha shughuli za kukuza ujasiriamali, biashara, uwekezaji wa miradi na mapendekezo ya sera ili kuimarisha mfumo wa ikolojia.

JICA Tanzania ilizindua shindano la pili la NINJA Januari 2022 (NINJA2) ili kuendelea kusaidia wafanyabiashara chipukizi na inafuraha kutangaza kukamilika kwa mafanikio kwa NINJA2.

Ikiwa ni hatua ya kwanza ya uteuzi wa NINJA2, biashara tatu za Kitanzania zilizoanzishwa ziliibuka washindi kutoka katika jumla ya waombaji 162 ambapo JICA iliendesha programu ya kuwajengea uwezo kwa muda wa miezi mitano.

Kisha, hatua ya mwisho ya uteuzi, biashara mbili kati ya tatu zilioanzishwa zilichaguliwa kuwa washindi yaani, EcoAct Tanzania Limited na Agripoa Company Limited. JICA ilitoa fedha taslimu kwa biashara hizi mbili ili kusaidia shughuli zao za Uthibitisho wa Utekelezekaji wa Mawazo ya Biashara (PoC).

Kama sehemu ya mpango huo, biashara tatu zilizoanzishwa zilizochaguliwa katika hatua ya kwanza ya uteuzi ambapo zilipata nafasi ya kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo kulingana na mahitaji yao ya kitaalamu yaliyotambuliwa kupitia Deloitte Consulting Limited.

Promenade utilizing plastic lumbers manufactured by EcoAct.

Msaada wa kitaalamu ulijumuisha kufuatilia maendeleo yao, kuwashauri na kuwaelekeza katika utekelezaji wa PoC zao, marekebisho ya mipango yao ya PoC na tathmini ya shughuli zao za biashara. Kupitia msaada wa kitaalamu, wamehamasishwa kuboresha biashara zao na wameweza kukuza uwezo wao kwa kuboresha miundo na kufafanua mikakati ya biashara pamoja na kuboresha mbinu za uuzaji.

Zaidi, biashara hizo zilipata fursa ya kufanya uwasilishaji kwa wadau wa Japan (wakiwemo: kampuni za Japan, wawekezaji wa Japan, n.k.) na wadau wa Tanzania wakiwemo wadau wa mfumo wa ikolojia za uanzishaji wa biashara.

Kulingana na mafunzo ya uboreshaji wa mbinu za biashara zao na mkakati wa mafunzo ya kujenga uwezo, kampuni mbili zilizotunukiwa tuzo zilitekeleza shughuli za PoC kwa miezi mitano. Ziliweza kuboresha uendeshaji na kupanua biashara zao. Februari 2023, JICA ilichapisha makala za video za shughuli zao ili kukuza ujasiriamali wao na pia kuongeza ufahamu kuhusu NINJA.

1. EcoAct Tanzania Limited

<Wasifu wa kampuni>

EcoAct Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2018 ni taasisi ya kijamii iliyojikita katika kushughulikia changamoto za uchafuzi wa plastiki baada ya matumizi, udhibiti wa taka, uchafuzi wa bahari, ukataji miti na mabadiliko ya tabianchi. EcoAct hutumia teknolojia bunifu ya uchakataji wa plastiki inayoitwa “Waxy 2” kuchakata taka za plastiki na kuzigeuza kuwa mbao za plastiki. Mbao za plastiki ni mbadala rahisi na wa bei nafuu wa mbao pia hupunguza hitaji la vifaa vya ujenzi na samani zinazotengenezwa kwa mbao.

EcoAct hutumia asilimia 100 ya taka za plastiki zilizorejeshwa tena kiwandani ili kutengeneza mbao za plastiki zinazodumu, nafuu, na rafiki wa mazingira kwa ajili ya matumizi ya ujenzi utengenezaji wa samani, uzio hadi usanifu wa mazingira. Ikileta bidhaa zinazojali zaidi mazingira kwenye soko na zenye sifa za kipekee, teknolojia ya EcoAct inahakikisha kwamba mbao zake za plastiki zilizotengenezwa haziozi, zinastahimili mchwa, haziingii maji na hudumu zaidi ya miaka 40 bila kubadilishwa iwe zinatumika katika maeneo makavu au yenye unyevunyevu.

<Mpango wa NINJA>

Programu za mafunzo ya kuwajengea uwezo zimeiwezesha EcoAct kuandika mpango mkakati wa kuongoza mipango ya muda mrefu ya taasisi na uendeshaji ili kufikia malengo yake ya muda mrefu na kufafanua malengo na matarajio yake katika masharti ya kibiashara yanayoweza kupimika. Hivyo, taasisi itaweza kuwa na mipango iliyobuniwa ya robo mwaka na ya mwaka mzima inayohusishwa na mkakati wake wa biashara.

Zaidi ya hayo, EcoAct inaandaa mkakati wa masoko ambao utatoa ufafanuzi zaidi kuhusu wasifu wa wateja, njia bora za uuzaji, wadau wakuu wa kushirikiana na ni mifumo gani ya kidijitali itakayofaa zaidi kwa wateja wake. Kupitia programu za mafunzo ya kujenga uwezo, kampuni imetambua mwelekeo katika suala la kuwa na uwezo wa kuvutia mwekezaji mwingine ili kusaidia kukuza biashara.


(Makala ya video ya EcoAct)


2. Agripoa Company Limited

<Wasifu wa kampuni>

Agripoa ni Programu tumishi ya Usimamizi wa Mashamba inayotumia Akili Bandia kusaidia wafugaji wa kuku wa Kiafrika kupanga, kufuatilia na kuchanganua shughuli za ufugaji kwa msaada wa maarifa yanayotokana na data ili kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Agripoa ilianza na wafugaji wa kuku lakini inapanga kufikia mifugo mingine, kilimo cha bustani na mazao.

App hii hutumiwa na wafugaji kugundua ugonjwa wa kuku na hutoa ushauri juu ya hatua za kuchukua, pamoja na dawa. Pia inaruhusu mkulima kuzungumza na mtaalamu wa kilimo na kurekodi shughuli na gharama za kilimo za kila siku.

Kwa sasa, Agripoa App inapatikana kwenye jukwaa la Android. Watumiaji wa simu za janja za Android wanaweza kupakua App hiyo kupitia Google Play Store. Programu inawawezesha wakulima kufanya yafuatayo;

1. Kupata taarifa za soko ikiwa ni pamoja na kuunganishwa na soko, kutambua bidhaa zenye mahitaji makubwa sokoni, ubora wa bidhaa zinazohitajika katika soko husika na mahitaji na viwango vya wanunuzi.

2. Kupata maarifa na uchanganuzi wa taarifa za shamba ili uweze kujua maendeleo ya shamba, kupata kalenda ya chanjo, kujua kiasi cha chakula cha kulisha mifugo na kupata taarifa kuhusu milipuko mipya ya magonjwa na jinsi ya kuitibu.

3. Kupata maarifa kutoka kwa wataalamu kupitia mawasiliano na madaktari wa mifugo, kupata ufumbuzi wa magonjwa ya kuku na kubadilishana mawazo na wafugaji wengine.

4. Usimamizi wa mapato na matumizi kwa kufuatilia fedha zilizotumika kununua vyakula vya mifugo, dawa na pembejeo nyingine za shambani na kupokea taarifa ikiwa kuna matumizi yaliyopitiliza.

Farm Management Sofware of Agripoa.

<Mpango wa NINJA>

Kupitia programu za kuwajengea uwezo, Agripoa imeweza kubaini mikakati ya kuongeza mvuto na kusimamia uendeshaji na mipango yake ili huduma zake nyingine ziwe kibiashara kwa ajili ya kuongeza mapato. Kampuni pia imeweza kuandaa mpango mkakati wa miaka mitatu ili kuongoza shughuli na mipango yake. Zaidi, Agripoa ilifanikiwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Jubilee kutoa huduma za bima kwa wakulima ambao wamesajiliwa kupitia App yake.


(Makala ya video ya Agripoa)

Kuhusu Mradi wa NINJA】