Kijani Bond ya CRDB: Uwekezaji rafiki kwa mazingira unaokupa faida ya asilimia 10.25

WazirI wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo akipokea kitabu cha taarifa ya uwekezaji kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa tatu kulia), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (wa pili kulia), Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Mary Mniwasa na Mwakilishi wa Benki Kuu

Kutoka kwenye kutenga asilimia moja ya faida yake kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi ya mazingira, kuzindua program kwa ajili ya kuwezesha miradi ya uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hadi sasa kuuza hatifungani za kijani zenye faida kubwa, hii inamaanisha kuwa hakuna benki inayojali mazingira kama Benki ya CRDB.

Hatifungani ya Kijani iliyozinduliwa hivi karibuni (yaani Kijani Bond) na Benki ya CRDB ndiyo hatifungani yenye faida kubwa ya mazingira kuwahi kutokea si tu nchini bali Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kuzinduliwa kwa hatifungani ya Kijani ya Mpango wa Muda wa Kati unaoruhusu uwekezaji wa Sarafu za Mataifa Mbalimbali wenye thamani ya Dola za Marekani 300 milioni, kunaashiria hatua kubwa katika kufikia malengo ya Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha Tanzania 2020/21 – 2029/30, mwongozo wa kimkakati wa kuziwezesha sekta za umma na binafsi kwa ajili ya ustawi mkubwa wa watu.

Hatifungani ya kijani ya Benki ya CRDB inamhakikishia mwekezaji faida ya kiwango cha riba ya asilimia 10.25 kwa mwaka, faida ya juu zaidi ambayo huwezi kupata kutoka katika taasisi nyingine za fedha.

Pia, kiwango cha riba hulipwa mara mbili kwa mwaka, baada ya kila miezi sita, na kumfanya mwekezaji kuwa na uhakika wa kurudisha fedha zake ndani ya muda mfupi. Dirisha la uwekezaji limefunguliwa Agost 31 na litafungwa Oktoba 6, 2023. Baada ya hapo, hatifungani hiyo itaorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Habari njema ni kwamba tangu kuzinduliwa kwa hatifungani hiyo tayari imewavutia wawekezaji wengine mashuhuri duniani, ikiwa ni pamoja na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC), mwanachama wa Benki ya Dunia, linalokusudia kuwekeza asilimia 40 ya jumla ya thamani iliyopo, Dola za Marekani 300 milioni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Hatifungani ya Kijani (Kijani Bond) ya Benki ya CRDB.

Hii inaendelea kuipa benki hiyo sifa njema na imani kutoka kwa watu kwa kuwa miongoni mwa taasisi za fedha ambazo zimethibitishwa kuwa imara na salama kwa ajili ya uwekezaji, ikiwa ni viwango vilivyotolewa na moja ya wakala wa viwango vya taasisi za fedha duniani, Moody`s Investors Services. Mbali na hilo, benki hiyo pia imeshatajwa kuwa benki bora nchini na taasisi nyingine zinazotambulika duniani kama Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (GCF), Global Finance na Jarida la Euromoney katika nyakati tofauti.

Benki ya CRDB inatazamia kukusanya kiasi cha hadi Sh40 bilioni kutoka kwenye uwekezaji wa hati fungani hiyo (na ziada ya hadi Sh15 bilioni) katika awamu hii ya kwanza, jambo ambalo linaendelea kuwapa nguvu wawekezaji watarajiwa katika uwekezaji huu unaovutia zaidi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo ambaye alihudhuria hafla ya uzinduzi wa kihistoria wa hatifungani hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi, pamoja na viongozi wengine waalikwa, alipongeza hatua hiyo iliyopigwa na Benki ya CRDB, akisema kuwa ni uwekezaji endelevu katika nyakati hizi ambazo benki hiyo inaendelea kufungua milango ya fursa za mafanikio ya soko la mitaji na dhamana nchini. "Benki ya CRDB tayari imekuwa mfano wa kuigwa," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hatifungani ya Kijani (Kijani Bond).

Aidha, Waziri Mkumbo alisisitiza azma ya Serikali katika kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwa kuimarisha sera, sheria na kanuni zilizopo.

Akifafanua zaidi kuhusu dhana iliyopo kuhusu hatifungani hizo, Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa hatifungani hiyo ipo kwa ajili ya kila mtu. "Huu ni uwekezaji ambao hata mtu wa kawaida anaweza kushiriki na kufaidika, kwa uwekezaji wa awali wa Sh 500, 000 tu," aliongeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na wadau wengine waliochangia kuidhinishwa kwa hati fungani hiyo, alisema; “Benki ya CRDB mara nyingi imekuwa mwanzilishi wa huduma mbalimbali.” Dk Laay pia alidokeza kuwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wana fursa ya kufaidika na hatifungani hii, kwani inatoa fursa ya kuwekeza kwa sarafu mbalimbali.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana Tanzania (CMSA), Nicodemus Mkama aliipongeza Benki ya CRDB kwa kufikia hatua hiyo ya kihistoria na kukidhi matakwa ya viwango vya kimataifa vya hati fungani. “Tunatarajia kwamba hatifungani ya kijani itakuwa muhimu katika kuendeleza uwezeshaji fedha wa utekelezaji wa miradi inayohusu mazingira nchini,” alisisitiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Mipango, Profesa Kitila Mkumbo (wa tano kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk. Laay (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa CRDB Foundation, Martin Warioba (wa kwanza kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (wa nne kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tano kulia), katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi, Dk Fred Msemwa (wa pili kushoto), Boniface Mhegi (wa tatu kulia) na Miranda Naiman (wa pili kulia) na Katibu wa Benki hiyo, John Rugambo (kushoto).

Mkurugenzi wa Masoko ya Mitaji, FSD Africa  Evans Osano alisema kuwa uuzaji wa hatifungani hizo za kijani unaakisi ukuaji wa kasi wa uchumi wa kijani nchini na inatoa fursa kubwa ya uwekezaji kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. "Ikiwa ni hatifungani ya kwanza ya kijani kutolewa nchini, huu ni wakati muafaka wa kusaidia kusukuma mbele ajenda ya uchangiaji fedha kwa ajili ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi barani Afrika na tunajivunia kutoa msaada wa kiufundi,” Bw Osano aliongeza.

Uuzaji wa hatifungani ya kijani unadhihirisha umakini wa Benki ya CRDB katika kuzingatia kanuni za mazingira, jamii, na utawala bora (ESG), na hivyo kuimarisha nafasi yake ya kuwa mdau mkuu katika uchangiaji fedha kwa ajili ya ulinzi wa mazingira.


Jinsi ya kuwekeza kwenye hati fungani ya kijani ya Benki ya CRDB

Ili kuwekeza, unapaswa kutembelea tawi la Benki ya CRDB lililo karibu nawe au wakala aliyeidhinishwa na CMSA. Hapo utapewa fomu ya uwekezaji katika Kijani Bond na kujaza taarifa zako ikijumuisha akaunti ya mwekezaji (CDS). Ikiwa hauna akaunti ya CDS utasaidiwa kufungua, utahitajika kutoa TIN namba, namba ya NIDA, na picha za pasipoti ili kufungua akaunti ya CDS.

Baada ya kujaza maelezo katika fomu ikijumuisha kiasi unachotaka kuwekeza, utahitajika kuhamisha/ kuweka kiasi unachotaka kuwekeza kwenye akaunti ya Hatifungani ya Kijani (inapatikana katika fomu).

Kwa wale wanaoishi nje ya nchi, unaweza kupakua fomu ya Kijani Bond kutoka tovuti rasmi ya Benki www.crdbbank.co.tz, na mara tu unapojaza fomu na kutuma kiasi cha uwekezaji, utahitajika kuwasilisha fomu hiyo kupitia barua pepe: [email protected]. Kwa taarifa zaidi kuhusu Kijani Bond wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB kupitia nambari ya bure 0800008000 au barua pepe [email protected].