Kwa nini ujiunge na familia yaSimBanking, miamala kidijitali
Katika watu wazima zaidi ya asilimia 65 wanaotumia huduma za benki nchini, ni wateja wa Benki ya CRDB pekee wanaofurahia ura¬hisi wa Programu ya Sim¬Banking ndiyo wanatambu¬lika duniani. Ndio, huu ni ukweli unaothibitika.
Programu ya SimBank¬ing ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa upati-kanaji wa huduma za Benki ya CRDB kwenye simu za mkononi, imetambuliwa kuwa programu salama zaidi ya benki kwenye tuzo zilizotolewa hivi karibuni na Jarida la Global Finance lenye makao makuu yake nchini Uingereza.
Benki ya CRDB ilikuwa kati ya taasisi tatu za fed¬ha kutoka Afrika zilizot-ambuliwa na kutunukiwa katika tuzo za mwaka huu zilizotolewa na jarida hilo maarufu duniani. Taasisi nyingine zilikuwa Benki ya Dashen ya nchini Ethiopia na First National Bank ya Afrika Kusini.
Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi wa Uhariri wa Jarida la Global Finance, Joseph Giarraputo anas¬ema washindi wa kip¬engele cha programu bora ya benki walipatikana kwa kuzingatia aina ya hudu¬ma wanazozitoa kidijitali, mafanikio waliyoyapata kwa kuwahamishia wateja wao kwenye huduma za kidijitali, uandikishaji wa wateja wapya sambamba na kuwabakiza wale wa mwanzo, na namna majuk¬waa ya kidijitali yalivyotu¬mika kuboresha biashara, kupunguza gharama na kuongeza tija.
“Kila mshiriki alijadiliwa na jopo la wataalamu wa huduma za benki na mifu¬mo ya TEHAMA kutoka Infosys, lakini uamuzi wa mwisho ulifanywa na jopo la majaji wetu wa Global Finance. Kutoka Tanzania, Benki ya CRDB imeshinda kwa kuwa benki ya kidiji¬tali,” amesema Giarraputo.
Benki nyingi barani Afri¬ka, Giarraputo anasema zimekuwa zikipitia wakati mgumu kutokana na chan¬gamoto za kiuchumi kwe¬nye mataifa yao hata hivyo, mikakati iliyowekwa na baadhi ya taasisi hizi za fedha imezisaidia kuk¬abiliana nazo na kuzifanya zivuke salama.
“Badala ya kuanguka na kufilisika kutokana na ugu¬mu uliopo, bado benki hizi zinaendelea udumu na baa¬dhi zinapata faida kubwa hivyo kustahili pongezi,” anasema mkurugenzi huyo wa uhariri wa Jarida la Global Finance.
Mchango wa SimBanking
Mpaka Jarida la Global Finance linatoa tuzo hiyo kwa Benki ya CRDB, taarifa zinaonyesha mafanikio makubwa ya Programu ya SimBanking kwani imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha matu¬mizi ya huduma za kidijitali ndani ya taasisi hii kubwa zaidi ya fedha nchini ikihu¬dumia pia Burundi na Jam¬huri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Boma Raballa, Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB ambayo mpaka Sep¬temba 2024 thamani ya mali zake ilikuwa shilingi trilioni 16, anasema benki imeshin¬da tuzo mbili mwaka huu. Ya pili ni benki bora ya kidi¬jitali.
Kupitia SimBank¬ing ambayo imefanyiwa maboresho kadhaa tangu ilipozinduliwa mwaka 2009, Raballa anasema wateja wa Benki ya CRDB wanapata huduma karibu zote waka¬ti wote na wakiwa mahali popote jambo lililosaidia kuongeza ujumuishi wa wananchi katika huduma za kidijitali.
“Tumepandisha ukomo wa fedha ambazo mteja anaweza kukamilisha mia¬mala yake kupitia SimBank¬ing. Mwanzoni ilikuwa Sh 5 milioni lakini sasa hivi ni Sh 10 milioni. Kiasi hiki kip¬ya kinawawezesha wateja wengi kukamilisha mambo yao kwa wakati. Mteja pia anaweza kuomba mkopo kupitia simu yake na kupata huduma nyingine nyingi,” anasema Raballa.
Kutokana na urahisi wa kutumia, Programu ya Sim¬Banking imekuwa na manu¬faa kwa wateja wa nchini hata wanaoishi nje ya Tan¬zania jambo lililoongeza tija na ufanisi kama inavyothibi¬tishwa na taarifa za fedha za robo ya tatu mwaka 2024 wa Benki ya CRDB.
Taarifa hizo zinaonyesha mikopo iliyotolewa ime¬ongezeka kutoka Sh 8.1 tril¬ioni Septemba 2023 mpaka Sh 10.1 trilioni Septemba 2024. Ongezeko hili la miko¬po limetokana na kuimarika kwa amana za wateja zilizo-panda kutoka Sh 8.7 trilioni mpaka Sh 10.3 trilioni ndani ya kipindi hicho.
Mpaka Septemba 2024, Benki ya CRDB ilipata faida ya Sh 583.9 bilioni kabla ya kodi ikilinganishwa na Sh 411.4 bilioni zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana. Baada ya kuli¬pa kodi, faida hiyo imebaki Sh 408.9 bilioni ikipanda kutoka Sh 280.5 bilioni ya mwaka jana. Faida hii ilito¬kana na matumizi sahihi ya mali za Benki zenye tha-mani ya Sh 16 trilioni amba¬zo zimepanda pia kutoka Sh 12.8 trilioni zilizokuwapo Septemba 2023.
Matumizi ya majukwaa ya kidijitali yakiongozwa na SimBanking ndani ya Benki ya CRDB yamekuwa na mchango mkubwa kati¬ka utoaji na usimamizi wa mikopo. Kwa sasa, Mkuru¬genzi wa Wateja Wadogo na wa Awali wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul anasema mteja anaweza kuomba mkopo kupitia programu hiyo na akaupata kwenye simu yake wakati huohuo.
Wanaoweza kupata mkopo kwa utaratibu huo, Bonaventura anasema ni wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopokea mkopo kutoka Bodi ya Miko¬po ya Elimu ya Juu (HES¬LB) pamoja na wastaafu na marejesho yao yanakatwa kwenye akaunti zao tarehe itakapofika.
Kwa watumiaji wote wa SimBanking, anasema upo mkopo wa Jinasue unaoleng akumwezesha mteja kununua umeme, kulipa bili ya maji au kulipia king’amuzi chake na pale inapobidi anaweza akapata fedha taslimu kati ya shi¬lingi 1,000 mpaka shilingi milioni moja.
Kutokana na usimam¬izi mzuri unaochangiwa, pamoja na mambo mengine, matumizi ya Programu ya SimBanking, ukwasi wa Benki ya CRDB umeongeze¬ka kutoka Sh 1.58 trilioni zilizokuwapo Septemba 2023 mpaka Sh 2.722 trilioni mwaka huu.
Katika kipindi hicho, ben¬ki ilipata Sh 321.16 bilioni kutokana na ada na kamish¬eni. Kiasi hiki kinachochan¬giwa na mapato yatokanayo na huduma za SimBanking kilipanda kutoka Sh 257.76 bilioni zilizopatikana mwa¬ka jana.
Wananchi kuzawadiwa na SimBanking
Wakati SimBanking pamoja na majukwaa men¬gine yakizifanya huduma za Benki ya CRDB kupatikana kidijitali kwa zaidi ya asil¬imia 96, benki ilizindua na inaiendeleza kampeni inay¬olenga kuwazawadia wateja wanaofanya miamala mingi kupitia jukwaa hilo.
Bonaventure anasema mteja anaweza kulipa bili mfano ya maji au umeme, kufanya malipo serikalini, kulipia bidhaa dukani, vituo vya mafuta au vinywaji baa, kuuliza salio na men¬gine mengi bila kulazimika kwenda tawini hivyo kue¬puka usumbufu wowote ambao angeweza kukutana nao.
“Mteja anaweza kufungua akaunti kupitia SimBank¬ing. Lengo letu ni kuhakiki¬sha mteja anapata kila ana¬chokitaka mahali alipo na aende tawini kwa mahitaji ya vitu vichache sana vina¬vyohitaji maelezo ya ziada,” anasema Bonaventura na kuongeza: “Huduma nyingi kwa sasa zinafanyika kidiji¬tali duniani hivyo miamala nayo inahamia huko pia. Ni lazima nasi tuungane na dunia, tusiachwe nyuma. Nimwombe kila Mtanza¬nia kuhakikisha anajiunga na Benki ya CRDB ili kutu¬mia huduma hizi salama na zenye uhakika.”
Kupitia kampeni ya Ben¬ki ni SimBanking yenye kaulimbiu ya ‘swahiba, miamala inalipa,’ inayo¬lenga kusajili wateja wapya pamoja na kukamilisha usajili wa wateja waliopo ambao hawatumii huduma hii, Bonaventura anasema wateja hushinda zawadi za aina tofauti kutokana na miamala wanayoifanya kila siku.
Zawadi hizo, anasema zinajumuisha gari aina ya Nissan Dualis ambayo ndio kubwa zaidi, linalotolewa kila baada ya miezi miwili, bajaji moja na pikipiki mbili zinazotolewa kila mwezi, simu 10 za kisasa kila mwezi, kompyuta mpakato 10 kila mwezi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, na fedha taslimu kiasi cha shilingi 30,000 zinazotolewa kwa washindi 32 kila mwezi.
“Wateja wanaotumia huduma za SimBanking wana nafasi kubwa zaidi ya kuibuka washindi. Nawasihi waendelee kufanya miamala mingi kupitia SimBanking ili kujishindia moja kati ya zawadi hizi hivyo kunufaika zaidi,” anasihi Bonaventura.
Licha ya zawadi za aina tofauti zinazotolewa, wate¬ja wa SimBanking sasa wanaweza kupata hudu¬ma bure wakipiga USSD kwa kubofya *150*03# ili kufurahia huduma wazita¬kazo tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo ilihitaji kuwa na muda wa maongezi ili kufanya miamala uita¬kayo.
Ili kutoa nafasi kwa wate¬ja wengi zaidi kujishindia zawadi hizi, Benki ya CRDB imeanza ziara ya kuhamasi¬sha matumizi ya SimBank¬ing kwa Watanzania wote tangu Novemba 15 ikipita katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.