Makala za video za kampuni tatu changa zenye ubunifu

Muktasari:

  • Mwaka 2020, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) lilizindua Shindano la Mpango wa Biashara liitwalo “NINJA (Ubunifu wa Siku za Usoni na Japan),” kama hatua ya kukabiliana na janga la Uviko-19.

Mwaka 2020, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) lilizindua Shindano la Mpango wa Biashara liitwalo “NINJA (Ubunifu wa Siku za Usoni na Japan),” kama hatua ya kukabiliana na janga la Uviko-19.

JICA iliandaa shindano la mpango wa biashara wa kikanda barani Afrika uitwao “NINJA”, ili kuvumbua miundo na teknolojia bunifu za biashara ambazo sio tu hutoa masuluhisho dhidi janga la sasa la Uviko-19 lakini pia kukabiliana na mabadiliko makubwa yanayotarajiwa ya kijamii na kiuchumi yanayosababishwa na janga hilo.

Mpango wa NINJA ulilenga kampuni changa bunifu zinazokua kwa kasi na taasisi kutoka nchi 19 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Nchini Tanzania, kampuni tatu ziliibuka washindi wa shindano hilo la NINJA.

Ofisi ya JICA Tanzania ilifanya tathmini ya utekelezekaji wa mawazo ya biashara ambayo yatapunguza athari na/au yenye uwezo wa kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika hiki kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19, ikiambatana na tuzo za washindi kati ya Februari hadi Oktoba 2021.

Januari 2022, JICA ilichia makala maalumu ya video (iliyorekodiwa/iliyohaririwa na Trickster Limited<http://trickster-africa.com/>) ikibeba mjumuisho wa shughuli za kampuni tatu zinazokuwa kwa kasi ili kukuza ujasiriamali nchini, na kuongeza ufahamu kuhusu NINJA.

Makala za video za kampuni tatu changa zenye ubunifu

NINJA nchini

Nchini Tanzania, kampuni tatu changa zinazokuwa kwa kasi, Agrinfo Company Limited, Tanzania Maji Jibu Company Limited, na Toolboksi Technologies Limited, ziliibuka washindi kati ya kampuni 90 zilizowasilisha mawazo yao ya kibunifu katika shindano hilo.

Makala za video za kampuni tatu changa zenye ubunifu

Tanzania Maji Jibu Company Limited

Mwaka wa uanzishwaji: 2017

Jina la Mwanzilishi: Bw. Tayeb Noorbhai

Makao Makuu: Arusha

Biashara: Kutoa maji safi kwa maeneo ya vijijini / nafasi ya kazi kwa vijana

Tanzania Maji Jibu inawanufaisha na kuwawezesha wajasiriamali wachanga kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kunywa kwa gharama nafuu na mahitaji mengine kwa kutumia mtindo wa biashara za kushirikishwa (franchise).

Jibu imewawezesha wajasiriamali kuwekeza pamoja nao katika biashara kupata haki za kutumia nembo na jina lake kufanya biashara ya maji jambo linalorahisisha upatikanaji wa maji salama katika jamii zao. Wanatoa fedha kupitia mtindo wa biashara za kushirikishwa unaowapa wafanyabiashara wadogo faida kubwa ya biashara.

Katika kipindi hiki cha shindano la NINJA, Jibu limeongeza idadi ya biashara za kushirikikishwa nchini kufikia viwanda 20. Viwanda hivyo ni pamoja na Mianzini, Moshono, Ilala, Goba, Tanga na Tegeta vilianza kazi kupitia NINJA. Kutokana na hali hiyo, Jibu ilitengeneza ajira mpya 60 na kuwezesha kaya 3,000 kupata maji ya kunywa kwa bei nafuu, safi na salama.

Makala za video za kampuni tatu changa zenye ubunifu

Agrinfo Company Limited

Mwaka wa uanzishwaji: 2015

Jina la Mwanzilishi: Bi Rose Funja

Eneo Makao Makuu: Dar es Salaam / Site: Moshi

Biashara: Ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za kwa wakulima wadogo.

Kampuni ya Agrinfo ilibuni na kutengeneza suluhisho la jukwaa la kidijitali, “JembeKilimo” ambalo linaunganisha wakulima wadogo wadogo (SHFs) wafikiwe na huduma na vipengele muhimu vinavyoboresha uzalishaji wao ikiwa ni pamoja na taarifa za shughuli za kilimo cha kisasa.

Kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi, taarifa zote za kuaminika za shughuli za kilimo zinakusanywa kupitia picha za drone na satelaiti, kwa uchambuzi zaidi.

JembeKilimo hutoa taarifa za afya ya shamba kwa wakulima wadogo kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwa wakati ili kusaidia kukuza mavuno yenye tija. Kwa kuongezea, kampuni hii ilishinda nafasi ya 3 kama kampuni bora ya inayokua kwa kasi barani Afrika katika fainali ya Mashindano ya NINJA yaliyofanyika huko Tokyo, Februari 2021.

Makala za video za kampuni tatu changa zenye ubunifu

Toolboksi Technologies Limited

Mwaka wa uanzishwaji : 2018

Mwanzilishi : Julius J. Mbungo

Makao Makuu : Dar es Salaam

Biashara : Uoanishaji ujuzi na kazi na mafunzo kwa mafundi wanaofanya kazi za mikono.

Toolboksi ni jukwaa la teknolojia ya biashara ya mtandaoni ambalo huwapa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi (wanaoitwa mafundi au wabunifu wa kazi za mikono) fursa za kazi na mazingira wezeshi ya kuimarisha ujuzi wao kwa minajili ya kukuza fani. Inaunganisha kaya na biashara na watu wanaoaminika na waliothibitishwa kwa ajili ya kuhudumu mahitaji ya kimsingi ya matengenezo, uwekaji umeme na utunzaji.

Hivi sasa, Watanzania wanne kati ya watano wanaofanya kazi (yaani asilimia 80) wanategemea ajira zisizo rasmi kupata kipato na wanakabiliana na changamoto ya uaminifu na sifa stahiki kwa wateja wao.

Toolboksi husaidia kuongeza nafasi za ajira kwa watu wa sekta isiyo rasmi kwa kuongeza kipato chao na kuboresha maisha yao kupitia jukwaa lao la mtandaoni, huku wakitoa huduma bora kwa kaya na wafanyabiashara wanaotafuta mafundi wa kuaminika wa kufanya ukarabati, ufungaji wa mifumo ya umeme na huduma za matengenezo.


Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan

Ni shirika la usimamizi wa Misaada Rasmi wa Maendeleo (ODA) la Japani. Ni mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya misaada duniani yanayosaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi zinazoendelea duniani. Nchini Tanzania, JICA imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Tanzania kwa takriban miaka 60 katika sekta nyingi kama vile kilimo, viwanda, miundombinu n.k tangu 1962.


Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi:

Japan International Cooperation Agency (JICA) Ofisi ya Tanzania

Sanduku la Posta 9450, Dar es Salaam, Simu: 022-211327/30